TORRES atwaa BUTI ya DHAHABU!
Spain wameicharaza Italy bao 4-0 katika Fainali ya EURO 2012 iliyochezwa Uwanja wa Olimpiki huko Kiev, Ukraine na kuweka historia ya kuwa Nchi ya kwanza Barani Ulaya kuweza kutetea Taji lao ambalo walilipata kwenye EURO 2008 na pia kuwa Nchi ya kwanza Duniani kuweza kutwaa Mataji matatu makubwa mfululizo ambayo ni EURO 2008, Kombe la Dunia Mwaka 2010 na EURO 2012.
Spain walipata bao lao la kwanza katika Dakika ya 14 baada ya kazi njema ya Fabregas kuingia ndani ya boksi na kutia krosi ya juu na iliyounganishwa kwa kichwa na David Silva.
Bao la pili la Spain lilipatikana Dakika ya 41 baada ya wao kuunasa mpira kufuatia mashambulizi ya Italy na pasi ya mwisho toka kwa Xavi kumkuta Jordi Albi aliemalizia kitulivu.
Fernando Torres alipiga bao la 3 katika Dakika ya 84 na kumfanya atwae Buti ya Dhahabu kwa kuwa Mfungaji Bora wa EURO 2012 kwa kufunga Bao 3 sawa na Mario Gomez wa Germany lakini yeye amepata tuzo hiyo kwa vile tu ametoa msaada kwa wenzake kupata magoli na pia amecheza Dakika chache kupita Gomez ambacho ni kigezo cha UEFA ikiwa Wachezaji watafungana kwa Magoli.
Bao la 4 lilifungwa na Juan Manel Mata kattika Dakika ya 88 baada ya pasi ya Torres.
Mashabiki wakishangilia

Baloteli jana hakufua dafu
Matukio ya hapa na pale uwanjani kabla ya mtanange kuanza jana usiku
Mashabiki wakishangilia
mashabiki wakiendeleza mbwembwe uwanjani
Mashabiki
No comments:
Post a Comment