Villas-Boas, Miaka 34, alifukuzwa na Chelsea Mwezi Machi baada ya kukaa hapo Miezi 9 tu, anategemewa kusaini Mkataba wa Miaka mitatu na upo uwezekano mkubwa yeye kutangazwa Meneja mpya hapo Jumanne.
Wiki iliyopita Makocha Kevin Bond na Joe Jordan walioletwa Spurs na Harry Redknapp walibwaga manyanga na hivyo kufungua njia kwa Villas-Boas kuwaleta Watu wake, José Mario Rocha na Daniel Sousato, ambao alikuwa nao tangu FC Porto na kuhamia nao Chelsea.
Na hata kabla AVB hajatua White Hart Lane Klabu hiyo tayari imechangamka kupata Wachezaji wapya kwa ajili ya Msimu mpya na wapo njiani kumnasa Gylfi Sigurdsson, Mchezaji wa Iceland, ambae Msimu uliopita alichezea Swansea City kwa mkopo akitokea Hoffenheim ya Germany.
No comments:
Post a Comment