BUKOBA SPORTS

Saturday, July 28, 2012

KAGAME CUP: FAINALI YANGA SC 2 V 0 AZAM FC - YANGA KIDUMEEE!

kikosi cha Azam
FAINALI ya Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, kati ya Yanga SC na Azam FC mtanange umemalizika hivi sasa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, YANGA yakijinyakulia ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Azam, baada ya kumalizika kwa mechi ya kusaka mshindi wa tatu, AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ikiifunga 2-1 APR ya Rwanda.
                                                   Kikosi cha timu ya Yanga
Mechi kati ya Yanga na Azam inachezeshwa na refa Thierry Nkurunzinza kutoka Burundi, akisaidiwa na Simba Honore wa Rwanda na Peter Sabatia wa Kenya, wakati mezani atakaa Issa Kagabo wa Rwanda, Kamisaa Hassan Amir wa Somalia na Mtathmini wa marefa ni Anangwe Robert wa Kenya.
Yanga SC; Ally Mustafa ‘Barthez’, Stefano Mwasyika, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Rashid Gumbo, Haruna Niyonzoma, Said Bahanuzi, Hamisi Kiiza na David Luhende. Benchi; Shamte Ally, Juma Seif, Ladislaus Mbogo, Idrisa Assenga na Jerry Tegete.
Azam FC; Deo Munishi ‘Dida’, Ibrahim Shikanda, Erasto Nyoni, Said Mourad, Aggrey Morris, Jabir Aziz, Kipre Tcheche, Salum Abubakar, John Bocco ‘Adebayor’, Ibrahim Mwaipopo na Ramadhan Chombo ‘Redondo’. Benchi; Mwadini Ally, Samir Haji Nuhu, Joseph Owino, George Odhiambo, Mrisho Ngassa, Khamis Mcha ‘Vialli’ na Gaudence Mwaikimba.Katika mchezo uliotangulia wa kusaka mshindi wa tatu, AS ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) iliifunga APR ya Rwanda mabao 2-1, mabao yake yakifungwa na Magola Mapanda dakika ya 18 na Mutombo Kazadi dakika ya 67, wakati la kufutia machozi la timu ya jeshi la Rwanda, lilifungwa na Jean Mugiraneza dakika ya 89. 

No comments:

Post a Comment