BUKOBA SPORTS

Tuesday, July 24, 2012

KAGAME CUP: SIMBA SC 1 - 3 AZAM FC - AZAM KWENDA NUSU FAINALI

Kikosi cha timu ya Simba
Mchezaji wa timu ya Simba ya Tanzania akijaribu kuondoka na mpira kuelekea golini mwa timu ya Azam FC katika mchezo naofanyika kwenye uwanja wa taifa jioni hii ikiwa ni michuano ya Kombe la Kagame, mpaka sasa timu ya Azam FC inaongoza magoli 2-1 dhidi ya timu ya Simba yaliyofungwa na mshabuliaji John Boko wakati lile la Simba limefungwa na Shomari Kapombe.Timu zikisalimiana hapa
SIMBA leo imetolewa katika michuano ya Kombe la Kagame baada ya kuchapwa mabao 3-1 na Azam katika mechi ya robo fainali iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mshambuliaji John Bocco ndiye aliyeibuka shujaa wa Azam baada ya kuifungia mabao yote matatu, moja kipindi cha kwanza na mengine kipindi cha pili. Bao pekee la Simba lilifungwa na Shomari Kapombe.
Ushindi huo umeiwezesha Azam kutinga nusu fainali, ambapo sasa itakutana na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Vita imefuzu kucheza hatua hiyo baada ya kuitoa Atletico ya Burundi mabao 2-1 katika mechi iliyochezwa kuanzia saa nane mchana.
Mechi nyingine ya nusu fainali itazikutanisha Yanga na APR ya Rwanda. Yanga imetinga hatua hiyo baada ya kuitoa Mafunzo ya Zanzibar kwa penati 5-3 wakati APR iliitoa URA ya Uganda kwa mabao 2-1.
Kwa mujibu wa ratiba, mechi zote mbili za nusu fainali zitachezwa Alhamisi wiki hii. Mechi ya kwanza itazikutanisha Azam na APR wakati katika mechi ya pili, Yanga itavaana na AS Vita.
Fainali ya michuano hiyo inatarajiwa kupigwa Jumapili, ikitanguliwa na mechi ya kutafuta mshindi wa tatu.
KIKOSI CHA AZAM KILICHOANZA
SIMBA_v_AZAM1. Deogratius Munishi (27) 2. Ibrahim Shikanda (21) 3. Erasto Nyoni (6) 4. Said Moradi (15) 5. Agrey Moris (13) 6. Kipre Bolou Michael (29) 7. Kipre Tchetche (10) 8. Salum Abubakar (8) 9. John Bocco (19) 10. Ibrahim Mwaipopo (4) 11. Khamis Mcha Khamis Viali (22)
KIKOSI CHA SIMBA SC KILICHOANZA
1: Juma Kaseja 2: Shomari Kapombe 3: Haruna Shamte 4: Juma Nyoso 5: Lino Masombo
6: Mussa Mudde 7: Jonas Mkude 8: Mwinyi Kazimoto 9: Felix Sunzu 10: Haruna Moshi1 1: Uhuru Suleiman 

No comments:

Post a Comment