JANA zilisambaa habari za kifo cha mcheza filamu mahiri, Eddie Murphy kwamba amefariki kwa ajali baada ya chombo cha moto maalum kwa ajili ya kutereza kwenye barafu alichokuwa akiendesha kupoteza mwelekeo na kugonga mti nchini Uswisi.
Hiyo ni mara ya pili kwa msanii huyo aliyetamba na filamu ya 'Coming to America' kuzushiwa kifo, ambapo Mei mwaka huu habari ilikuwa kama hivyo.
Mtandano wa www.mediafetcher.com, uliandika Murphy aliumia sehemu za kichwani ingawa alivaa kofia ya usalama 'Helmet', na huenda ajali hiyo ilichangiwa na mwendo kasi.
Tovuti hiyo ilidai kuwa, Murphy alikuwa kwenye mapumziko binafsi nchini Uswisi wakati akipata ajali hiyo, na upo uwezekano alifariki muda mfupi baada ya ajali.
Aidha, mitandao mingine ilikanusha taarifa za kifo cha Murphy na kusema taarifa hizo ni uzushi. |
|
No comments:
Post a Comment