BUKOBA SPORTS

Wednesday, July 25, 2012

KAMA ULIKOSA MKASI-SO3E10 WITH HAJI RAMADHANI

Haji Ramadhani bila shaka anakumbukwa na ataendelea kukumbukwa kama Haji wa BSS kwani kwenye Bongo Star Search ndipo unapoweza kupata chimbuko lake. Hadithi ya Haji ni mojawapo ya zile simulizi za kweli ambazo zinakwambia usikate tamaa kwani kesho huijui na mpangaji na muamuzi ni yeye aliyetuumba sote.Kutoka kwenye ufundi mchundo tu wa kawaida jijini Mwanza mpaka hivi sasa kuwa mwimbaji kiongozi katika bendi maarufu ya muziki nchini(Twanga Pepeta) yaweza kuwa ndoto iliyotimia kwa namna yake. Wiki iliyopita,yaani Jumatatu katika kipindi cha Mkasi,Haji aliketi na Salama,Mubah na Johnie katika Mkasi pale Amaya Beauty Salon & Spa katikakati ya Jiji la Dar-es-salaam. Aliongelea mengi lakini lipo moja ambalo bila shaka linaweza kukugusa na wewe pia.Wakati jamaa anahangaika kutafuta ushindi wa BSS,mwenzie aliyemwacha nyumbani naye alikuwa “busy” na mengine. Mtoto,ambaye kimsingi hana kosa,akazaliwa ambaye sio damu ya Haji.Jamaa akarudi,akasamehe na maisha yanaendelea na anaendelea kulea mwana asiye wake. Ni kisa cha aina yake.Msikilize mwenyewe Haji endapo kwa bahati mbaya hukupata kumsikiliza Jumatatu iliyopita.

No comments:

Post a Comment