Akionyesha kusikitishwa kwake huku akikiri Wachezaji kadhaa waliokuwemo kwenye Ziara hiyo hawakuwa fiti, Wenger alitamka: “Difensi yetu inaonekana bado dhaifu hasa kwenye Kipindi cha Kwanza na KitChee. Tuna kazi kubwa.”
Katika Mechi tatu ilizocheza huko Asia, Difensi ya Arsenal iliruhusu bao 5 pale ilipoifunga Kombaini ya Malaysia bao 2-1, ilipofungwa 2-0 na Manchester City na kutoka sare 2-2 na KitChee.
Wenger aliongeza: “Tuliruhusu kila Mtu acheze lakini baadhi hawajafikia kiwango cha Ligi Kuu. Wanajifunza. Kama hujifunzi kwenye Mechi hizi za kujipima huwezi tena, nimewapa nafasi wajue nini kinahitajika kwenye kiwango hiki cha juu. Niliwachezesha Madifenda wote lakini nyumbani wapo Madifenda wazoefu tuliowaacha, yupo Sagna, yupo Koscielny, yupo Mertesacker, wote hawa wazoefu wakubwa!”
Kwenye Mechi hiyo na Kitchee Difensi ya Mtu 4 ilianza na Kieran Gibbs, Johan Djourou, Ignasi Miquel na Craig Eastmond.
SORCE: SOKAINBONGO
No comments:
Post a Comment