Maicon
Chelsea wanahitajika kusajili beki wa kulia baada ya kuamua kumuweka Paulo Ferreira Sokoni huku Jose Bosingwa akiachiliwa kama mchezaji huru baada ya mkataba wake kuisha.
Maicon mwenye umri wa miaka 30 amekuwa akisifika kama beki wa kulia bora duniani kwa mda mrefu sasa na sasa anatarajiwa kuja kudhihirisha hivyo katika ligi ya Uingereza akiwa na Chelsea.
Anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitatu, huku akiwa anapokea mshahara wa paundi 80,000 kwa wiki.
No comments:
Post a Comment