BUKOBA SPORTS

Friday, July 27, 2012

KIRAFIKI: ARSENAL 0 V 2 MANCHESTER CITY MCHEZO ULIOCHEZWA LEO HUKO BEIJING!


Bao la kwanza la Man City lilifungwa na Pablo Zabaleta katika Dakika ya 41 na Dakika mbili baadae Yaya Toure akapiga bao la pili ambalo Arsenal walidai ni ofsaidi.
Kipindi cha Pili Alex Oxlade-Chamberlain wa Arsenal alikosa bao baada ya kugonga posti.
Arsenal walikuwa wakionekana wazuri kwenye Kiungo ambako Abou Diaby, Alex Song na Mikel Arteta walishirikiana vyema lakini pengo la Robin van Persie lilionekana waliposhindwa kuipenya ngome ya Mtu tatu ya Man City ya Kompany, Toure na Savic huku pembeni wakicheza Zabaleta na Alexander Kolarov na mbele yao Kiungo cha Mtu tatu cha Yaya Toure, Mchezaji toka Ivory Coast Abdul Razak na Nir Bito, anaetoka Israel.
Baada ya Mechi hii, Timu hizi zinaendelea Ziara zao za Bara la Asia kwa Man City kuelekea Malaysia na Arsenal kwenda Hong Kong.
VIKOSI
Arsenal: Fabianski, Jenkinson, Bartley, Vermaelen, Gibbs, Diaby, Arteta, Song, Andre Santos, Walcott, Gervinho.
Akiba: Szczesny, Oxlade-Chamberlain, Coquelin, Chamakh, Miyaichi, Yennaris, Eastmond, Miquel, Aneke, Eisfeld, Afobe.
Manchester City: Pantilimon, Zabaleta, Kompany, Toure, Savic, Kolarov,
Toure Yaya, Biton, Razak, Tevez, Aguero.
Akiba: Holmen Johansen, Adam Johnson, Suarez, Boyata, Scapuzzi, Lopes, Evans.
Refa: Howard Webb [England]

No comments:

Post a Comment