Wednesday, July 25, 2012

MTANANGE WA KIRAFIKI WA SHANGHAI SHENHUA VS MANCHESTER UNITED WAMALIZIKA, SHINJI KAGAWA AIFUNGIA MAN U GOLI 1-0

Shinji Kagawa akitupia
LEO Manchester United wameifunga Shanghai Shenhua bao 1-0, bao alilofunga Shinji Kagawa likiwa ndio bao lake la kwanza tangu ajiunge, katika Mechi iliyochezwa huko Mjini Shanghai, China na kufanikiwa kutwaa Chevrolet China Cup.
Shanghai ilicheza bila ya Wachezaji wao Nyota wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba na Nicolas Anelka, baada ya Kocha wa Timu yao, Sergio Batista kutoka Argentina, kuamua kuwapumzisha ili Jumamosi wacheze Mechi ya Ligi Kuu China ambayo Timu hiyo imekuwa haifanyi vizuri.
Bao la ushindi la Man United lilifungwa Dakika ya 68 na Shinji Kagawa baada ya kazi njema ya Bebe kwenye Winga ya kushoto.
Ferguson akifurahia mtanange wa timu yake leo hii.... 
 Kagawa akifanya mambo yake leo
KIKOSI CHA MAN UNITED: Lindegaard, Veseli, Ferdinand, Carrick, Brady, Anderson, Powell, Kagawa, Petrucci, Valencia, Macheda
Manchester United - ZIARA 2012
Julai 18 vs Amazulu FC ( Moses Mabhida Stadium, Durban, Afrika Kusini)==MATOKEO 1-0
Julai 21 vs Ajax Cape Town (Cape Town Stadium, Cape Town, Afrika Kusini) ==MATOKEO 1-1
Julai 25 vs Shanghai Shenhua (Shanghai Stadium, Shanghai, China)==MATOKEO 1-0
Agosti 5 vs Valerenga v Man United, Ullevall Stadium, Oslo, Norway
Agosti 8 vs Barcelona (Uwanja wa Ullevi, Gothenburg, Sweden)
Agosti 11 vs Hannover 96 (AWD Arena, Hannover, Germany- Chevrolet Cup)

1 comment:

  1. Tunakushukuru blogger kwa kutupa habari nyingi na nzuri sana ila habari za Man U zinazidi ktk blog yako wakati timu nyingi zinafanya matukio. Yaweza kuwa we ni mwanachama wa hiyo club ila balance habari.

    ReplyDelete