BUKOBA SPORTS

Saturday, July 7, 2012

PARK JI - SUNG AHAMIA QPR BAADA YA MAKUBALIANO KUKAMILIKA.

Queens Park Rangers wamefikia makubaliano na Manchester United kumnunua Kiungo Park Ji-sung kwa ada inayodhaniwa kuwa Pauni Milioni 5.
Park, Miaka 31, alihamia Man United Mwaka 2005 akitokea PSV Eindhoven na kucheza Mechi 133 za Ligi Kuu England na kufunga Bao 19 huku akitwaa Ubingwa wa Ligi mara 4 na UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Park alianza Soka lake la kulipwa huko Japan akicheza Klabu ya Kyoto Purple Sanga na aling’ara sana kwenye Kombe la Dunia la Mwaka 2002 alipoifikisha Nchi yake Korea kwenye Nusu Fainali ya Mashindano hayo yaliyochezwa kwa pamoja huko Korea na Japan.
Baada ya hapo akamfuata Kocha wa Timu ya Taifa ya Korea, Guus Hiddink, kwenye Klabu ya PSV Eindhoven ambako alichezea Miaka mitatu na kuchukuliwa na Manchester United kwa ada ya Pauni Milioni 4.

No comments:

Post a Comment