Usain Bolt.
MWANARIADHA nyota wa mbio fupi, Usain Bolt amesisitiza nia yake ya kutaka kufanya majaribio katika klabu ya Ligi Kuu nchini Uingereza ya Manchester United. Bolt raia wa Jamaica mwenye umri wa miaka 25 ambaye ni mwanariadha mwenye kasi zaidi katika historia ya mbio hizo alifanikiwa kutetea medali yake ya olimpiki baada ya kufanikiwa kushinda mbio za mita 100 akitumia sekunde 9.63 na kuvunja rekodi yake mwenyewe aliyoiweka katika michuano hiyo mwaka 2008 jijini Beijing. Lakini Bolt ambaye ni shabiki mkubwa wa klabu ya United ana matarajio kuwa huko mbele anaweza kubadili mwelekeo na kuamua kucheza soka.
Nyota huyo ambaye anatarajiwa kutetea medali yake katika mbio za mita 200 Agosti 9 mwaka huu, aliongeza kuwa bado yuko jijini London kwa siku kadhaa hivyo kama Ferguson atamhitaji anajua mahali pa kumtafuta.
kwa hisani ya blog beki3.blogspot.com
No comments:
Post a Comment