Sunday, August 26, 2012
CHELSEA WAMSAJILI MOSES
Victor Moses
Chelsea sasa wametumia zaidi ya paundi mil 80 katika kusajili wachezaji msimu huu.
Siku ya ijumaa wamekamilisha tena usajili wa mchezaji wa Wigan Victor Moses kwa ada ya paundi mil 9.
Chelsea ndiyo klabu iliyotumia hela nyingi sana katika usajili kuliko klabu yoyotempaka sasa katika ligi ya Uingereza ingawaje Di Matteo anasema bado klabu za Manchester ndizo anazipa kipaumbele katika kutwaa kombe.
Chelsea pia wanampango wa kuuza Malouda lakini kikwazo kinakujakatika mshara wa mchezaji huyo. Amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake na ameambiwa anaweza kuhama kwenda klabu nyingine lakini tatizo mchezaji huyo hataki kuhama halafu mshahara wake wa paundi 70,000 ukatwe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment