Lindegaard, mwenye Miaka 28 na aliejiunga na Man United Januari 2011, sasa atabakia hapo Klabuni hadi Mwaka 2016.
Akizungumzia Mkataba huu mpya, Lindegaard amesema: “Nimefurahi sana kusaini Mkataba mpya. Nimefurahi kuona Meneja anayo imani na mimi. Hakuna sehemu nyingine yeyote ninayotaka kuwepo zaidi ya hapa. Ushindani wa namba hapa Klabuni ni mkubwa na hii ndivyo inavyotakiwa kwa Klabu kama hii. Hii inatufanya sisi binafsi tuwe bora na, muhimu zaidi, inaifanya Klabu iwe imara zaidi.”
Nae Meneja wa Man United Sir Alex Ferguson amepokea vyema habari za Lindegaard kuongeza Mkataba na amesema: “Anders bado ni mdogo kwa Makipa lakini amepanda juu kiwango tangu afike hapa.
Upo ushindani mkubwa wa Makipa, na hili Siku zote ni kitu bora kwa Klabu, lakini kwangu mie naumia kichwa!”
No comments:
Post a Comment