BUKOBA SPORTS

Sunday, August 12, 2012

KIRAFIKI: MAN UNITED WAMALIZA ZIARA YAKE KWA KUIFUNGA GOLI 4 KWA 3 HANNOVER YA GERMANY

Wakicheza Mechi yao ya mwisho ya Ziara 2012 waliozuru Afrika Kusini, China, Norway, Sweden na Germany, Manchester United leo waliimaliza kwa kishindo na kutwaa Chevrolet Cup ndani ya AWD Arena, Hannover, Germany baada ya kutoka nyuma wakiwa wamefungwa bao 3-1 na Wenyeji Hannover 96 zikiwa zimebaki Dakika 24 na kuibuka Washindi wa Bao 4-3 huku Wayne Rooney na Shinji Kagawa wakiwa ndio Mashujaa.
Hannover ndiyo walitangulia kupata bao baada ya Kipa Lindegaard kuutema mpira na Artur Sobiech kumalizia lakini Man United wakasawazisha kwa bao la Chicharito.
Hadi mapumziko bao zilikuwa 1-1.
Kipindi cha Pili, Hannover walipiga bao mbili na kuwa mbele kwa bao 3-1 lakini Rooney akakomboa moja kwa frikiki tamu na kusawazisha kufanya bao ziwe 3-3 kwa Penati baada ya yeye mwenyewe kuangushwa na Kipa.
Zikiwa zimebaki Dakika 5 Rooney akamtolea pande kwa kichwa Shinji Kagawa ambae alifunga bao la 4 na la ushindi.
Michael Keane akipambana na adui
 David De Gea akitema mpira kwenye eneo la hatari
 Patrice Evra akichuana vikali na Adrian kuwania mpira
MAGOLI:
Dakika/Mfungaji
Hannover 96
25 Artur Sobiech
48 Karim Haggui
66 Mohammed Abdellaoue
Manchester United
31 Javier Hernandez ‘Chicharito’
69 Wayne Rooney
82 Wayne Rooney [Penati]
85 Shinji KAGAWA

KIKOSI
Man United: Lindegaard; M Keane, Carrick, Vidic, Evra; Nani, Cleverley, Kagawa, Young; Rooney, Hernandez
Akiba: De Gea, Ferdinand, Anderson, Brady, Bebe, Giggs, Valencia, Berbatov

kwa hisani:sokainbongo

No comments:

Post a Comment