PELE AKIWA NA MSHINDI WA MEDALI YA DHAHABU KATHERINE GRAINGER
Nchi hiyo ya amerika ya kusini inaandaa mashindano mawili kwa pamoja yaani kombe la dunia 2014 na mashindano ya olimpiki 2016 lakini mkongwe wa mchezo wa mpira wa miguu wa brazil pele ana wasiwasi kuhusu uwezekano wa brazil kuwa tayari kuandaa mashindano hayo makubwa kabisa duniani.
Mkongwe huyo wa soka ana wasiwasi kuhusu miundombinu ya nchi hiyo na kwamba miundombinu kama barabara na mambo mengine mengi hayajakamilika mpaka sasa na sidhani kama mambo yote yanaweza kukamilika kwa wakati kabla ya mashindano hayo kuanza.
Tuna matatizo katika ujenzi , tutajitahidi kuweka mambo sawa lakini tuna wasiwasi katika suala la mawasiliano kwa sababu hatuko sawa katika suala la mawasiliano na usafiri siyo mzuri.
watu wanasema tutafanikiwa lakini sina uhakika na hilo kwani tumebakiwa na miaka miwili tu kuweza kukamilisha mambo hayo.
Nimeongea na Rais Dilma na amesema atafanya kila liwezekanalo kuweka mambo sawa lakini hatuko tayari alimalizia kusema Pele.
No comments:
Post a Comment