BUKOBA SPORTS

Sunday, August 12, 2012

MANCHESTER CITY WATWAA NGAO YA JAMII BAADA KUILIZA CHELSEA GOLI 3-2


Pongezi kwenu CITY!!!!!!!!!!!!
Mancini akitembea huku amebeba ngao ya jamii....
Mabingwa wa Ligi Kuu England Manchester City leo wametwaa Ngao ya Jamii baada ya kuwafunga Mabingwa wa Ulaya, Chelsea, waliokuwa wakicheza Mtu 10 kuanzia Dakika ya 42, kwa bao 3-2 kwenye Mechi ya fungua dimba Msimu mpya wa Mwaka 2012/13 iliyochezwa Villa Park huko Mjini Birmingham.

 Fernando Torres akiipatia timu yake Chelsea goli la kwanza kabla ya mapumziko

Chelsea ndio walitangulia kupata bao katika Dakika ya 40 kufuatia ushirikiano mwema kati ya Ramires na Mata kisha Fernando Torres kutikisa nyavu
Lakini Dakika mbili baadaye Refa Kevin Fiend alimtoa kwa Kadi Nyekundu Beki wa Chelsea Ivanovic kwa kile kilichodaiwa rafu mbaya kwa Kolarov.
Baada ya refa kuachia kadi nyekundu wachezaji walimjia juu refa
wasalimie huko nje!!!

Yaya Toure akirudisha goli mara baada ya kipindi cha pili kuanza na kufanya 1-1

 Tevez akiipatia goli Man city dakika ya 59

Samir Nasri akifanya vitu vyake kutimiza goli 3-1dhidi ya Chelsea

Nasri akifurahia ushindi wake kwa timu yake!

Ryan Bertrand akiipatia goli la pili chelsea na kufanya matokeo yabaki 2-3
  Di Matteo(kushoto) na  Mancini (kulia)
Mashabiki wa City

No comments:

Post a Comment