West Brom wameshinda mbio hizo za kumsajili Lukaku mwenye umri wa miaka 19 baada ya kuzipiku klabu nyingi zilizokuwa zikimtaka ikwemo Fulham.
Lukaku ambaye alijiunga na Chelsea kwa ada ya paundi mil 18 msimu uliopita amejiunga na West Brom ambako atakuwa chini ya kocha msaidizi wa zamani Steve Clarke ambaye sasa ndiye kocha wa West Brom.
“Ninafuraha kukamilisha usajili huu. Baada ya msimu uliopita kuwa sio mzuri kwangu ninafuraha kuweza hakikishiwa kucheza sasa hapa West Brom.
Nimeskia mengi kuhusiana na Steve Clarke kwa hiyo nadhani itakuwa bora kwangu kumsikiliza na kujifunza kutoka kwake.” alisema Lukaku.
Steve Clarke nae hakukaa kimya alisema,
“Ninafuraha kumkaribisha Romelu kalbuni hapa.
Ananguvu na nimshambuliaji ambaye bado ni mdogo na ana uchu wa kujifunza na pia alikuwa na shauku ya kuja hapa kwa hiyo hilo ni la kushukuru.”
No comments:
Post a Comment