BUKOBA SPORTS

Wednesday, August 15, 2012

USAIN BOLT: KAMA ALEX FERGUSON ATANIHITAJI - NITAFANYA KILE NILICHOFANYA KWA RONALDO



Jina lake sasa linasikika dunia nzima kama mtu anayekimbia kwa spidi kuliko mtu yeyote duniani na sasa anataka kuushangaza ulimwengu kwa kuhama fani. “Watu wanafikiria ya kuwa natania ninaposema ya kuwa nataka kuchezea Manchester United.
Kama Alex Ferguson akiniita kwa ajili ya majaribio kamwe siwezi kataa.
Nsingetaka kufanya hilo kama siliwezi, najijua mie ni mchezaji mzuri na naweza saidia sana timu kwani ntakuwa mtu mwenye mbio sana na pia ntakuwa mchezaji.
Nahisi nilimsaidia sana Cristiano Ronaldo kuwa mchezaji bora” alisema Bolt baada ya kushinda medali yake ya dhahabu katika mbio fupi.Bolt alishawahi kwenda United ambako alikuwa akifanya mazoezi na Ronaldo na akaweza mfundisha hata jinsi ya kukimbia sana.Usain Bolt bingwa wa Olimpiki katika mbio za mita 100 ambaye ni raia wa Jamaika amesema kuwa, anataka kuchezea timu ya soka ya Manchester United ya Uingereza. Bolt amedai kwamba, aliwahi kusema hilo na sasa analikariri tena hilo kwamba, anapenda kuona siku moja anaichezea Man U. Watu wanadhania natania, lakini kama kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson ataniita kwa ajili ya majarabio, siwezi katu kukataa wito huo, amenukuliwa Usain Bolt na gazeti la The Sun. Wakati huo huo, mashindano ya Olimpiki yameendelea huko nchini Uingereza huku mchuano mkali wa medali ukiwa baina ya Marekani na China. Katika msimamo wa medali China ingali inaongoza ambapo hadi sasa imejipatia medali 31 za dhahabu, 19 za fedha na 14 za shaba. Marekani inainyemelea China kwa karibu mno ambapo imejikusanyia medali 29 za dhahabu, 15 za fedha na 19 za shaba. Wenyeji Uingereza wamejitutumia katika siku tatu hizi na sasa wanashika nafasi ya tatu katika msimamo wa medali baada ya kujipatia medali 18 za dhahabu, 11 za fedha na 11 za shaba. Afrika Kusini inashika nafasi ya 16 ikiwa na medali tatu za dhahabu na moja ya fedha na kuwa nchi ya kwanza katika msimamo wa nchi za Kiafrika katika mashindano hayo ya Olimpiki.

No comments:

Post a Comment