BUKOBA SPORTS

Friday, August 10, 2012

LUKAS MOURA AKUBALI KWENDA PSG

Paris Saint-Germain imethibitisha kumsaini Lucas Moura kutoka Sao Paulo kwa Dau la Euro Milioni 35 na Mchezaji huyo ataanza kuichezea Klabu yake hiyo mpya kuanzia Januari 2013.

Kwa muda mrefu Moura, Miaka 19, alikuwa akiwaniwa na Klabu za Manchester United na Inter Milan lakini PSG, inayomilikiwa na Kampuni ya Qatar, imeshinda baada ya kupandisha Dau.

PSG imetoa tangazo rasmi kwenye Tovuti yao ikithibitisha Uhamisho huu kwa kusema wao na Sao Paulo wamefikia makubaliano ya Uhamisho wa Moura na pia PSG na Moura zimesaini Mkataba wa Miaka minne kuanzia Januari 2013 hadi Julai 2017.

Moura anakuwa Mchezaji wa nne kusaini chini ya Meneja wa PSG Carlo Ancelotti kwa ajili ya Msimu mpya wengine wakiwa ni Mbrazil Thiago Silva, Straika Zlatan Ibrahimovic na Muargentina Ezequiel Lavezzi.

Moura kwa sasa yuko Uingereza na Kikosi cha Brazil ambacho Jumamosi kitacheza Fainali ya Mashindano ya Olimpiki dhidi ya Mexico.

No comments:

Post a Comment