BUKOBA SPORTS

Friday, August 10, 2012

ZENIT WAKARIBIA KUMSAJILI DIMITAR BERBATOV WA MANCHESTER UNITED


Berbatov
Timu ya Zenit St Petersburg inakaribia kukamilisha usajili wa mchezaji wa Manchester United Dimitar Berbatov limesema gazeti la Gazzetta dello Sport.
Berbatov mwenye umri wa miaka 31 anatarajiwa kuihama klabu yake ya Man United kutokana na kutopata nafasi za kucheza.
Klabu nyingi za Ulaya zikiwemo Bayern Munich, AC Milan na Galatasaray zote zimehusishwa na usajili wa mchezaji huyo lakini Zenit ndio inaonesha ya kuwa imeshinda mbio hizo.
Inasemekana mabingwa hao wa Urusi wapo katika mazungumzo na mchezaji huyo na wanauhakika kuwa usajili huo utafanyika.
Chanzo: talkSPORT

No comments:

Post a Comment