BUKOBA SPORTS

Saturday, August 11, 2012

MECHI YA MWISHO YA ZIARA 2012 KWA MAN UNITED KUCHEZWA LEO HUKO AWD ARENA, KATI YA HANNOVER YA GERMANY SAA 3:20 USIKU..

LEO Usiku huko Germany, Manchester United wanacheza Mechi yao ya mwisho ya ZIARA 2012 Uwanjani AWD Arena Mjini Hannover dhidi ya Wenyeji wao Hannover 96 na Mshindi atatwaa Chevrolet Cup.
Hii ni mara ya kwanza kabisa katika historia zao kwa Manchester United na Hannover 96 kukutana.
Juzi Alhamisi, Hannover 96 waliitwanga St Patrick’ s Athletics ya Ireland bao 2-0 katika Mechi ya marudiano ya Raundi ya Tatu ya EUROPA LIGI baada ya kuwapiga 3-0 katika Mechi ya kwanza.
Ushindi huo umewafanya Hannover 96 waingie Raundi ya Mchujo ya EUROPA LIGI na watacheza na Slask Wroclaw.
Hannover 96 itacheza bila Mchezaji wa zamani wa Man United, Mame Biram Diouf, ambae ameumia lakini wanae Kipa Ron-Robert Zieler aliewahi kuwa Old Trafford.
Msafara wa Man United kwenda huko Ujerumani una Wachezaji 19 wakiwemo Ryan Giggs na Tom Cleverley ambao wanaungana na Timu yao kwa mara ya kwanza baada ya kuwa kwenye Michezo ya Olimpiki na Team GB.
KIKOSI KAMILI:
De Gea, Lindegaard; Evra, Ferdinand, M Keane, Vidic; Anderson, Bebe, Robbie Brady, Michael Carrick, Tom Cleverley, Ryan Giggs, Nani, Valencia, Young; Berbatov, Hernandez, Kagawa, Rooney.

Manchester United - ZIARA 2012:
Julai 18 vs Amazulu FC ( Moses Mabhida Stadium, Durban, Afrika Kusini)==MATOKEO 1-0
Julai 21 vs Ajax Cape Town (Cape Town Stadium, Cape Town, Afrika Kusini) ==MATOKEO 1-1
Julai 25 vs Shanghai Shenhua (Shanghai Stadium, Shanghai, China)==MATOKEO 1-0
Agosti 5 vs Valerenga v Man United, Ullevall Stadium, Oslo, Norway)==MATOKEO 0-0
Agosti 8 vs Barcelona (Uwanja wa Ullevi, Gothenburg, Sweden)==MATOKEO 0-0, Penati 0-2
Agosti 11 vs Hannover 96 (AWD Arena, Hannover, Germany- Chevrolet Cup) )==SAA 3 Dak 20 Usiku

KWA HISANI YA SOKAINBONGO

No comments:

Post a Comment