BUKOBA SPORTS

Saturday, August 11, 2012

KOCHA WA JUVENTUS ANTONIO CONTE ACHOMWA MIEZI 10 KWA TUHUMA ZA UPANGAJI WA MATOKEO

Kocha wa Juventus Antonio Conte amefungiwa Miezi 10 baada ya kuhusishwa na tuhuma za upangaji matokeo Mechi na yeye akidaiwa kuwa alishindwa kutoa ripoti kuhusu uhalifu huo wakati akiwa na Klabu ya Siena katika Msimu wa Mwaka 2010/11 kwenye Ligi ya Serie B.

Msimu uliopita, uliomalizika Mwezi Mei, ukiwa Msimu wake wa kwanza na Juventus, Conte, Miaka 43, aliiongoza Klabu hiyo kutwaa Ubingwa wa Serie A bila kufungwa hata Mechi moja.
WASIFU wa Antonio Conte
•Kuanzia Mwaka 1991, aliichezea Juventus Mechi 400 za Ligi

•Akiwa na Juve kama Kiungo, alishinda Ligi mara 5 na Kombe la Ulaya

•Conte aliichezea Italy mara 35

•Mbali ya Juventus na Siena, Conte pia aliwahi kuwa Kocha wa Arezzo, Bari na Atalanta.

No comments:

Post a Comment