BUKOBA SPORTS

Saturday, August 11, 2012

OLIMPIKI LONDON 2012: FAINALI LEO JUMAMOSI BRAZIL V MEXICO KUCHEZWA UWANJA WA WEMBLEY JIJINI LONDON SAA 11 JIONI

LEO Jumamosi Saa 11 Jioni Uwanja wa Wembley Jijini London utakuwa na Fainali ya Wanaume ya Mashindano ya OLIMPIKI LONDON 2012 ambayo Mshindi wake hutwaa Medali ya Dhahabu kati ya Mexico na Brazil, Nchi ambayo imetwaa kila Taji kubwa Duniani, yakiwemo Kombe la Dunia mara 5 na Copa America mara 8, lakini hadi leo hawajapata Medali ya Dhahabu ya Olimpiki huku mara ya mwisho kucheza Fainali ya Olimpiki ikiwa ni Mwaka 1988, Fainali waliyoongozwa na Bebeto na Romario, lakini wakaambulia Medali ya Fedha.
Kocha wa Mexico Luis Fernando Tena atalazimika kuziba pengo la Giovanni dos Santos kwa kumchezesha Javier Cortes.
Kocha wa Brazil Mano Menezes yeye hana upungufu wa Wachezaji na anategemewa kuchezesha Kikosi kile kile kilichoitwanga Korea ya Kusini bao 3-0 kwenye Nusu Fainali isipokuwa Alex Sandro kubadilishwa na Marcelo kucheza huku Kiungo wa Chelsea, Oscar, akiendelea kuhaha nyuma ya Mastraika wao watatu Leandro Damiao, Hulk na Neymar.
VIKOSI VINAVYOTARAJIWA KUANZA
Brazil (4-3-3): Neto, Rafael, Thiago Silva, Juan, Marcelo, Romulo, Sandro, Oscar, Hulk, Leandro, Neymar
Mexico (4-2-3-1): Corona, Israel, Reyes, Araujo, Chavez, Enriquez, Salcido, Aquino, Herrera, Fabian, Peralta

No comments:

Post a Comment