Monday, August 27, 2012
RAIS KIKWETE AHESABIWA KATIKA SENSA YA WATU NA MAKAZI
Sensa ya watu na makazi ilianza jana nchini nzima kwa mafanikio makubwa licha ya changamoto kadhaa
kujitokeza, ikiwamo baadhi ya watu, hususan waumini wa dini ya Kiislamu kususia kushiriki kwa madai ya kutokuwapo kwa kipengele cha dini katika madodoso ya sensa.
Rais Jakaya Kikwete (kushoto) akiwa amepokea fomu kutoka kwa Kamishna wa Sensa Tanzania, Amina Mrisho, tayari kuhesabiwa katika Sensa ya Watu na Makazi nyumbani kwake Ikulu, Dar es Salaam leo. Rais na familia yake walihesabiwa kwa siri na Karani wa Sensa, Clement Ngallaba. Rais Kikwete na mkewe Mama Salma wakiondoka kwenda chumba maalumu kwa ajili ya kuhesabiwa
Rais Jakaya Kikwete akihamasisha wananchi kujitokeza kuhesabia mara baada ya kutoka kuhesabiwa yeye na familia yake, nyumbani kwake Ikulu, Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni mkwewe Mama Salma Kikwete.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa na familia yao, wakati Rais Kikwete akihojiwa na kujibu maswali kutoka kwa karani wa sensa ya watu na makazi, Clement Ngalaba, Rais alipojiunga na mamilioni ya Watanzania katika zoezi hilo lililoanza kufanyika leo Agosti 26, 2012, nchi nzima.
PICHA NA IKULU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment