BUKOBA SPORTS

Thursday, August 2, 2012

ROBERTO CARLOS DA SILVA ASTAAFU KUCHEZA SOKA

MCHEZAJI wa Brazil Roberto Carlos da Silva ametangaza rasmi kuacha kucheza Soka kama ilivyothibitisha Klabu yake Anzhi Makhachkala ya Urusi ambayo imesema atapewa wadhifa mwingine ndani ya Klabu hiyo.
Carlos, Miaka 39, ambae ameichezea Brazil Mechi 125, hajacheza Klabuni hapo tangu Mwezi Machi jina lake llipoondolewa kwenye Kikosi cha Wachezaji.
Kocha wa Anzhi Makhachkala, Guus Hiddink, amesema Roberto Carlos, aliejiunga na Anzhi Makhachkala Februari Mwaka 2011, atapewa wadhifa mwingine hapo Klabuni.
Mwenyewe Carlos amesema anatayarisha Mechi maalum ya kuaga ambayo itachezwa kati ya Anzhi Makhachkala na Klabu yake ya zamani Real Madrid.

HISTORIA
1991–1993 União São João-Mechi 33 Magoli 10

1993–1995 Palmeiras-Mechi 44 Magoli 3

1995–1996 Inter Milan-Mechi 30 Magoli 5

1996–2007 Real Madrid-Mechi 370 Magoli 46

2007–2009 Fenerbahçe-Mechi 65 Magoli 6

2010–2011 Corinthians-Mechi 35 Goli 1

2011–2012 Anzhi Makhachkala-Mechi 29 Magoli 4
JUMLA MECHI-Mechi 606 Magoli 75
BRAZIL
1992-2006 Mechi 125 Magoli 11
source:sokainbongo

No comments:

Post a Comment