JOSE MOURINHO AKIWA NA KOMBE LA UBINGWA WA UINGEREZA AKIWA NA CHELSEA
JOSE MOURINHO AKIWA NA KOMBE LA SCUDETO ALILOSHINDA AKIWA NA INTER MILLAN
JOSE MOURINHO AKISHEREHEKEA LA LIGA NA REAL MADRID
ALISHINDA TAJI LA ULAYA AKIWA NA FC PORTO NA INTER MILLAN
Kocha wa timu ya real madrid Jose mourinho anatarajia kulifuta jina lake la ''SPECIAL ONE'' na kuliboresha na sasa anataka aitwe ''ONLY ONE".
Jose mourinho anajisikia fahari na anaona anastahili kubadilisha jina lake baada ya kuwa kocha wa kwanza katika historia ya soka kuweza kunyakua vikombe mbalmbali akiwa na Timu za vilabu vikubwa vitatu barani ulaya na ligi kuu bora tatu barani ulaya.
Meneja huyo kutoka ureno ameshinda kombe la La Liga akiwa na real mdrid msimu uliopita na kuongeza taji jingine katika mataji aliyokuwa nayo awali akiwa na Inter millan na taji la uingereza mara mbili akiwa na Timu ya chelsea pamoja na kushinda mataji mbalimbali akiwa na klabu ya Porto ya nchini ureno bila kusahau mataji mara mbili ya ubingwa barani Ulaya.
Kutokana na sabau hizo sasa baada ya Special One watu sasa waanze kuniita ONLY ONE na kusahau jina la SPECIAL ONE
No comments:
Post a Comment