Saturday, August 25, 2012
TAMASHA LA FIESTA LAZINDULIWA KWA KISHINDO MJINI MOSHI.
Prezoo akiwarusha mashabiki kibao (hawapo pichani) waliojitokeza usiku wa kumakia leo kwenye uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Pichani juu na chini ni mwanamuziki kutoka nchini Kenya na mmoja wa shiriki wa shindano la Big Brother Stargame,CMB Prezoo akitumbuiza jukwaani usiku huu kwenye uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya uwanja wa chuo cha ushirika mjini Moshi.
Mmoja wa wasanii wa hip hop Joh Makini akikamua vilivyo usiku huu mbele ya umati mkubwa wa watu uliojitokeza kwenye uzinduzi wa tamasha la Fiesta.
Msanii mahiri wa bongofleva,Lina akiwa na densaz wake wakilishambulia jukwaa vilivyo.
Lina akiimba wimbo wake Yalaiti.
Mkali mwingine wa hip hop Mwana FA akishusha mitindo huru.
Pichani juu na chini Mwana FA akilishambulia jukwaa vilivyo kwa mitindo yake huru iliyokuna vilivyo mashabiki wake,waliofika kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Wasanii wa nyota wa Filamu hapa nchini nao walijumuika kwa pamoja kwenye uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012,pichani jukwaani ni Wema Sepetu,Jacob Steven a.k.a JB,pamoja na Aunt Ezekiel wakilisakata sebene.
Ray nae akilisakata sebene vilivyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment