BUKOBA SPORTS

Sunday, August 26, 2012

SIR ALEX FERGUSON: VAN PERSIE NI MOTO, ROONEY NJE WIKI 4! MAN U 3 FULHAM 2

RVP: ‘Najisikia niko nyumbani!’
Sir Alex Ferguson amesema Robin van Persie atazidi kuwa bora kadri muda unavyokwenda na amemsifia kwa kufunga bao lake la kwanza kwa Klabu yake Manchester United ambalo aliliita bao zuri sana lakini akatoboa kuwa Wayne Rooney atalazamika kukaa nje ya Uwanja kwa Wiki 4 baada ya kuchanika pajani.
Akimzungumzia Robin van Persie ambae amejiunga na Man United Wiki iliyopita akitokea Arsenal na kucheza Mechi yake ya kwanza Jumatatu iliyopita dhidi ya Everton ambayo alicheza kwa Dakika 22 za mwisho na leo kucheza Mechi nzima Uwanjani Old Trafford dhidi ya Fulham na kufunga bao moja katika ushindi wa bao 3-2, Sir Alex alisema:“Ni goli safi sana, alimalizia vizuri. Linadhihirisha uwezo wake wa kufunga mabao. Bao lake liliwainua Wachezaji wenzake na kuanza kucheza vizuri.”
Ferguson pia alisema kuwa Robin van Persie atazidi kuwa bora kadri muda unavyokwenda kwa kuzidi kuzoeana na wenzake.
Hata hivyo, Ferguson alikerwa na bao la pili la Fulham ambalo Man United walijifunga wenyewe kufuatia Nemanja Vidic na Kipa David de Gea kujichanganya wenyewe na Vidic kuingiza mpira wavuni.
ROONEY
Ferguson alithibitisha kuwa Wayne Rooney atakuwa je kwa Wiki 4 baada ya kuchanika pajani akimkabili Straika wa Fulham Hugo Rodalega ambae stadi za buti yake ndizo zilizomkata vibaya Rooney.
Rooney alianza Mechi hiyo akiwa benchi na kuingizwa kuchukua nafasi ya Shinji Kagawa.
Kuumia kwa Rooney kutamfanya azikose Mechi za England za Makundi kuwania kuingia Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 ambazo England itacheza na Moldova na Ukraine Septemba 7 na 11 na pia huenda akaikosaMechi ya kwanza ya Man United ya Kundi la UEFA CHAMPIONZ LIGI ambazo Mechi zake zitaanza kuchezwa katikati ya Septemba.Tukio lenyewe la Rooney kuumia 
“Ameenda Hospitali na inaonesha umeumia vibaya sana. Itabidi tuwe waangalifu sana kuhusiana na kidonda hicho lakini ameenda katika hospitali bora kwa hiyo naimani baada ya kama wiki nne hivi atakuwa amepona.
Ilikuwa ni bahati mbaya, Rodallega alikuwa anataka kucheza mpira.” alisema Fergie

Rodallega Akimpa pole Rooney
Fergie hakusita pia kumpa sifa Van Persie ambaye jana alifunga goli lake la kwanza.
“Palikuwa na ofa nyingi za kumtaka lakini akaamua kuja kwetu, na hapo inaonesha yeye sio mchezaji anayependa fedha ila anahusudu mpira, maana ukizungumza swala la fedha hakuna atakaye ipita Man City.”

Rooney akienda hospitali
ROBIN VAN PERSIE 
Akiongea mara baada ya Mechi na Fulham iliyochezwa Uwanjani Old Trafford, hiyo ikiwa mara yake ya kwanza kuanza Mechi na Manchester United na kucheza Uwanja huo na pia kufunga bao lake la kwanza kwa Klabu yake mpya aliyojiunga nayo Agosti 15, Robin van Persie ametamka: “Tangu siku ya kwanza kila Mtu amenikaribisha vyema. Wachezaji wote, Wafanyakazi na Mashabiki pia. Hata Jijini Manchester, Watu ni wakarimu kwangu.Ni Wiki moja tu, inabidi tuzoeane na Wachezaji wenzangu lakini tutazoeana. Najisikia nyumbani, niko poa.”
Pia, van Persie, akiongelea ushindi kwa Fulham, amesema kitu muhimu ni kupata Pointi 3 na yeye amefurahi kwa kufunga bao zuri.Goli la vidic kujifunga

No comments:

Post a Comment