Jana mechi za ligi kuu za England ziliendelea na kulikuwa na mechi nyingi tu na ligi hiyo ilikumbwa na kashikashi ya mvua kubwa baadhi ya maeneo.
Wamecheza Mechi tatu za Ligi Kuu England, kila Mechi wakipata na kufunga Penati, sasa wameshinda Mechi zote hizo tatu na wako kileleni, na hao si wengine ni Mabingwa wa Ulaya Chelsea ambao leo wakicheza kwao Stamford Bridge wameichapa Newcastle bao 2-0.
Torres alifanyiwa ndivyo sivyo hapa na kusababisha benati
Chelsea walipata bao lao la kwanza katika Dakika ya 22 kwa Penati iliyopigwa na Mchezaji wao mpya Eden Hazard na bao lao la pili katika Dakika ya 45 kwa bao la Fernando Torres baada ya kutengenezewa na Eden Hazard.Hazard akichonga penati
Mechi inayofuata kwa Chelsea ni huko Monaco hapo Agosti 31 kugombea UEFA Super Cup dhidi ya Atletico Madrid ambao ni Mabingwa wa EUROPA LIGI.
Kocha wa Newcastle Pardew (katikati) akijione kwa macho yote mawili timu yake ikipigwa 2-0
Hazard na Torres wakifurahia ushindi wao jana
VIKOSI:
Chelsea: Cech, Ivanovic, Luiz, Cahill, Cole, Mikel, Meireles, Bertrand, Hazard, Mata, Torres
Akiba: Turnbull, Essien, Romeu, Ramires, Lampard, Oscar, Sturridge.
Newcastle: Krul, Simpson, Coloccini, Steven Taylor, Santon, Ben Arfa, Cabaye, Anita, Gutierrez, Ba, Cisse
Akiba: Harper, Williamson, Perch, Ryan Taylor, Amalfitano, Marveaux, Obertan.
Refa: Phil Dowd
RATIBA:
Jumapili Agosti 26
[Saa 9 na Nusu Mchana]
Stoke City v Arsenal
[Saa 12 Jioni]
Liverpool v Manchester City
Jumamosi Septemba 1
[Saa 8 Dak 45 Mchana]
West Ham United v Fulham
[Saa 11 Jioni]
Swansea City v Sunderland
Tottenham Hotspur v Norwich City
West Bromwich Albion v Everton
Wigan Athletic v Stoke City
[Saa 1 na Nusu Usiku]
Manchester City v Queens Park Rangers
Jumapili Septemba 2
[Saa 9 na Nusu Mchana]
Liverpool v Arsenal
[Saa 12 Jioni]
Newcastle United v Aston Villa
Southampton v Manchester United
No comments:
Post a Comment