BUKOBA SPORTS

Friday, August 31, 2012

TAREHE YA MWISHO YA USAJILI LEO: TIMU NYINGI ZASAJILI KUIMARISHA TIMU ZAO KWA MSIMU 2012-2013

lleo ndiyo siku ya mwisho ya usajili nchini Uingereza.
Inasemekana Chelsea wanataka muuza Sturridge na kumnunua mchezaji Schurrle wa Bayer Leverkusen kwa ada ya paundi mil 8.

Arsenal inasmekana inataka mchukua Essien kwa mkopo leo kabla dirisha halijafungwa.
Nigel De Jong katua Italia kwa ajili ya kujiunga na AC Milan.
“Nafurahaa kuwa hapa na AC Milan ni klabu kubwa” amesema Jong.

Charlie Adam amewasili uwanja wa mazoezi wa Stoke anafanya mazungumzo na Kocha wa Stoke Tony Pulis.
Inasemekana anahama kwa ada ya paundi mil 4 mpaka 5.

Fiorentina baada ya kumkosa Berbatov na Bendtner sasa wanafanya maongezi na Ryan Babel.
Southampton wataka msajili  Mjapan Maya Yoshida.
Mwenyekiti wa Liverpool inasemekana amepiga simu Chelsea ili kukamilisha usajili wa mkopo wa Daniel Sturridge
Taarifa: Wachezaji wote kama watahitajika cheza kesho basi lazima usajili ukamilike mchana ila ukifanyika usiku basi haruhusiwi cheza kesho.
Mdogo wa Hazard arudi nchini kwao katika klabu ya Zulte kwa mkopo akitokea Chelsea.
Van Der Vaart anasemekana yupo njiani kujiunga na Hamburg.
Breaking News: Aston Villa wametoa paundi mil 7 kwa ajili ya Dempsey na hela yao imekubaliwa  kimbebe kwa Liverpool na Sunderland maana nao pia wanamtaka.
Berbatov kuna uwezekano akatua Tottenham badala ya Fulham.
Danny Rose wa Tottenham anakamilisha kuhamia Sunderland kwa mkopo.
Bendtner anakamilisha usajili wake wa kutua Juventus.
Liverpool wameambiwa wanaweza msajili Damiao kwa mkopo na kisha kumsajili moja kwa moja mwisho wa msimu kwa ada ya paundi mil 13.
Afellay ajiunga na Schalke kwa mkopo akitokea Barcelona.
TAYARI: Jay Spearing wa Liverpool ajiunga na Bolton kwa mkopo.
 TAYARI: De Jonga ajiunga na AC Milan
TAYARI: Kieran Richardson amejiunga na Fulham akitokea Sunderland

Richardson
14:25
TAYARI: Scott Sinclair akamilisha uhamisho wake kwenda Man City.


Sinclair
TAYARI: Charlie Adam ajiunga na Stoke City

adam
TAYARI: Danny Rose ajiunga na Sunderland kwa mkopo akitokea Tottenham.

Danny Rose
Tottenham wamfuatilia kiungo wa kireno Mountinho kwa ajili ya kuziba pengo la Modric.

Moutinho
Carroll akiwasili mazoezini West Ham kwa mara ya kwanza.

Andy Carroll Andy Carroll amejiunga na West Ham kwa mkopo wa mwaka mzima
TAYARI: Arsenal wamuuza Park Chu-Young kwa Celta Vigo.
TAYARI: Maicon amejiunga na Man City.

Maicon
TAYARI: Giovani dos Santos ameihama Tottenham nakujiunga na Real Mallorca kwa mkataba wa miaka minne.
Tottenham wamekubali kutoa paundi mil 22 kwa ajili ya kumnasa Joao Mountinho wa kutokea Porto.
Stephane Mbia yupo njiani anaenda jiunga na QPR.
Man City wajiandaa kuwasajili Javi Garcia kwa £20m na Matija Nastasic kwa £12m ukamilisho utakamilika baadaye.
Rafael van der Vaart amekubaliana na Hamburg kuhusiana na maswala ya mshahara na sasa mchezaji huyo anajiandaa kwenda kufanya vipimo.
Inasemekana helicopter ametua Craven Cottage (uwanja wa Fulham). Je Dimitar Berbatov ndo yumo ndani??
Winga wa Valencia Hernandez yupo QPR akifanya vipimo kwa ajili ya kukamilisha usajili wake.
TAYARI: van der vaart amekamilisha usajili wake wa Hamburg.

Van der Vaart
Roque Santa Cruz (unamkumbuka huyo) anafanyiwa vipimo Malaga.
TAYARI: Dimitar Berbatov ni mchezaji wa Fulham sasa.

Berbatov
Liverpool wapo tayari kumuuza Henderson kwa Stoke City kwa ada ya paundi mil 8. Nicklas Bendtner amehama Arsenal na kwenda kujiunga na Juventus ya ItaliaTAYARI: Man City wamsajili Javi Garcia kwa ada ya paundi mil 15.8 akitokea Benfica.
Javi Garcia
TAYARI: Wamsajili mshambuliaji Christian Benteke kutoka klabu ya Genk kwa ada ya paundi mil 7.
TAYARI: Real Madrid wamsajili Essien kwa mkopo.
TAYARI: Everton wamemsajili Bryan Oviedo kwa mkataba wa miaka minne akitoka FC Copenhage. Paundi mil 3.5 ndio fedha zilizotumika
Bryan Oviedo
TAYARI: Stoke wamemsajili Steven Nzonzi toka Blackburn kwa ada ya paundi mil 3.5
       MWISHO ....DIRISHA LIMEFUNGWA SAA 6.00 USIKU

No comments:

Post a Comment