BUKOBA SPORTS

Saturday, September 8, 2012

COASTAL UNION WAITUNGUA GOLI 1-0 DHIDI YA ZIMAMOTO


 WAENDELEZA WIMBI LA USHINDI ZBAR

Coastal Union
BAO pekee la Jerry Santo kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar jana  limeipa ushindi wa 1-0 Coastal Union katika mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Zimamoto.
Huo ulikuwa mchezo wa pili kwa Coastal katika ziara yao ya siku tano visiwani humo,
kujiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inayoanza wiki ijayo. Katika mchezo wa
kwanza, mabingwa hao wa Bara 1988, waliichapa Super Falcon mabao 3-0, wafungaji Suleiman
Kassim ‘Selembe’, Jerry Santo na Danny Lyanga na Jumapili Coastal watacheza mechi yao ya
mwisho na Mafunzo.
Wimbi hili la ushindi kwa Cosatal, linafuatia mwendo wa kusuasua kwenye michezo ya kirafiki
ya awali, ilipofungwa mechi nne kati ya tano, kiasi cha kuibuka tetesi makocha Juma Mgunda
na Msaidizi wake, Habib Kondo wanaweza kutupiwa virago.
Ilifungwa na Azam FC 2-0 Uwanja wa Chamazi, ilifungwa 2-1 na Yanga Uwanja wa Taifa,
ilifungwa 3-2 na Bandari mjini Mombassa, baadaye 2-0 Tanga, ilifungwa 2-1 na Polisi mjini
Morogoro na yenyewe iliifunga JKT Oljoro 1-0 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
source bin zubeiry

No comments:

Post a Comment