DEREVA WA LANGALANGA AFUNGIWA KUTOZWA FAINI KWA KUSABABISHA AJALI.
DEREVA wa magari ya kwenda kasi ya Langalanga wa timu ya Lotus, Romain Grosjean amefungiwa mara moja kushiriki mashindano ya magari hayo baada ya kusababisha ajali katika kona ya kwanza ya michuano ya Grand Prix nchini Ubelgiji. Grosjean raia wa Ufaransa mwenye miaka 26 ambaye amehusika katika ajali saba za mzunguko wa kwanza katika mashindano 12 msimu huu pia ametozwa faini ya paundi 40,000 kwa tukio hilo. Dereva huyo alimchomekea dereva wa MacLaren, Lewis Hamilton mwanzoni mwa mashindano hayo na kusababisha magari hayo kugongana na kuharibika vibaya ingawa kahuna mtu aliyejeruhiwa kwenye tukio hilo. Grosjean ambaye ni dereva wa kwanza kufungiwa kushiriki shindano moja toka Michael Schumacher alipopewa adhabu kama hiyo mwaka 1994 amesema kuwa alitazama vibaya umbaliuliokuwepo kati yake na Hamilton akidhani kuwa alikuwa tayari amempita dereva huyo lakini haikuwa hivyo. Dereva huyo aliomba radhi kwa tukio hilo lililosababisha ajali mbaya lakini cha muhimu anashukuru hakuna aliyeumia kati yao.
Button finished in first ahead of Sebastian Vettel and Kimi Raikkonen
McLaren's British star Jenson Button (katikati) wakishangilia ushindi huo kwenye podium
No comments:
Post a Comment