Liverpool v Arsenal
Hii ni BIGI MECHI kati ya Timu mbili ambazo hazijashinda Msimu huu.
Msimu uliopita Liverpool walifungwa nad Arsenal Bao 2-1, kwa bao za Robin van Persie, lakini safari hii Van Persie yupo Man United na itabidi wawategemee Wachezaji wao wapya, Lukas Podolski na Olivier Giroud, kuwapa Magoli.
Mechi hii, kwenye Winga moja, itawakutanisha Vijana wapya hatari, Winga mdogo wa Liverpool, Raheem Sterling, atakaepambana na Beki chipukizi Carl Jenkinson.
Hii ni Mechi nzuri na pengine Arsenal wataziona nyavu kwa mara ya kwanza Msimu huu baada ya kutoka sare za 0-0 katika Mechi zao mbili za kwanza huku Liverpool wakisaka ushindi wao wa kwanza baada ya kufungwa na kutoka sare katika Mechi zao.
Hali za Wachezaji:
Liverpool
Beki Daniel Agger ruksa kucheza Mechi hii baada ya kutumikia Kifungo cha Mechi moja kufuatia Kadi Nyekundu lakini Kiungo kutoka Brazil Lucas hatacheza na atakuwa nje ya Uwanja kwa Miezi miwili hadi mitatu baada ya kuumia paja.
Mbali ya hao, Meneja wa Liverpool, Brendan Rodgers, ana Kikosi chake kamili cha kuchagua Timu yake:
Reina, Kelly, Flanagan, Enrique, Johnson, Skrtel, Coates, Robinson, Carragher, Agger, Gerrard, Downing, Shelvey, Henderson, Allen, Cole, Suarez, Sterling, Borini, Morgan, Jones.
Arsenal
Beki Laurent Koscielny amerudi Kikosini baada ya kupona maumivu ya mguu lakini Kipa Wojciech Szczesny bado haijajulikana kama ataweza kucheza baada ya kuumia mbavu.
Majeruhi wa muda mrefu ambao hawapo Kikosini ni Kiungo Jack Wilshere (enka) na Beki Bacary Sagna (alivunjika mguu).
Meneja Wenger anaweza kupanga Timu yake kutokana na Kikosi kifuatacho:
Szczesny, Jenkinson, Vermaelen, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Diaby, Cazorla, Walcott, Arteta, Podolski, Gervinho, Fabianski, Arshavin, Ramsey, Giroud, Santos, Djourou, Coquelin.
Refa: Lee Probert
MSIMAMO WAKE ULIVYO KWA SASA KABLA YA MECHI ZA LEO
| P | W | D | L | GD | PTS | |
| Chelsea | 3 | 3 | 0 | 0 | 6 | 9 |
| Swansea | 3 | 2 | 1 | 0 | 8 | 7 |
| West Brom | 3 | 2 | 1 | 0 | 5 | 7 |
| Man City | 3 | 2 | 1 | 0 | 3 | 7 |
| Everton | 3 | 2 | 0 | 1 | 1 | 6 |
| West Ham | 3 | 2 | 0 | 1 | 1 | 6 |
| Wigan | 3 | 1 | 1 | 1 | 0 | 4 |
| Fulham | 3 | 1 | 0 | 2 | 1 | 3 |
| Man Utd | 2 | 1 | 0 | 1 | 0 | 3 |
| Stoke | 3 | 0 | 3 | 0 | 0 | 3 |
| Newcastle | 2 | 1 | 0 | 1 | -1 | 3 |
| Sunderland | 2 | 0 | 2 | 0 | 0 | 2 |
| Arsenal | 2 | 0 | 2 | 0 | 0 | 2 |
| Tottenham | 3 | 0 | 2 | 1 | -1 | 2 |
| Norwich | 3 | 0 | 2 | 1 | -5 | 2 |
| Reading | 2 | 0 | 1 | 1 | -2 | 1 |
| Liverpool | 2 | 0 | 1 | 1 | -3 | 1 |
| QPR | 3 | 0 | 1 | 2 | -7 | 1 |
| Southampton | 2 | 0 | 0 | 2 | -3 | 0 |
| Aston Villa | 2 | 0 | 0 | 2 | -3 | 0 |
Kwa hisani ya sokainbongo
No comments:
Post a Comment