BUKOBA SPORTS

Thursday, September 13, 2012

INIESTA NAYE NJE WIKI MBILI(2) KUJIUGUZA MISULI

Staa wa Barcelona, Andres Iniesta, Mchezaji Bora Ulaya, atakuwa nje kwa Wiki mbili akijiuguza maumivu baada ya kuumia musuli ya mguu wake wa kulia Spain ilipocheza na Georgia juzi kwenye Mechi ya Kundi I la kufuzu Fainali za Kombe la Dunia na kushinda 1-0.
Ingawa alicheza Dakika zote 90 za Mechi hiyo na Georgia, Klabu yake Barcelona imethibitisha Iniesta hatacheza kwa Wiki mbili.
Pigo hilo kwa Barcelona litamfanye Staa huyo kuzikosa Mechi za Klabu yake za La Liga dhidi ya Getafe na Granada na ile ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na Spartak Moscow.
Mchezaji mwingine wa Barca ambae huenda akaikosa Mechi ya Barca ya Jumamosi na Getafe ni Fulbeki wao Jordi Alba ambae anaumwa Flu.

No comments:

Post a Comment