Kikosi cha Kagera suger 2012Msimu mpya wa ligi kuu Tanzania Bara kwa mwaka 2012/2013 unaanza kutimua vumbi leo hii tarehe 15/9/2012 ambapo mshindi mtetezi Simba atakuwa nyumbani kukipiga na timu Arica Lyon kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Pazia la msimu huu mpya wa ligi hii ulifunguliwa rasmi siku ya jumanne kwa mechi ya Ngao ya jamii baina ya bingwa mtetezi na mshindi wa pili wa ligi hiyo iliyopita ambaye ni Azam Fc. Ambapo simba waliibuka kidedea kwa kuifunga Azam fc goli 3-2 na kunyakua ngao hiyo.
Huko uwanjani mkwakwani jijini Tanga timu ya Coastal Union timu ya Mgambo Shooting zitamenyena vikali na zote zinatoka eneo moja hilo hilo.
Mechi nyingine ni Police Morogoro iliyopanda daraja msimu itawakaribisha Mtibwa Suger kwenye uwanja wa Jamhuri.
JKT Ruvu itacheza na Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Mla Ndizi Kibaha - Pwani.

TOTO African wataikaribisha JKT Oljoro kwenye uwanja wa CCM kirumba. Wao Kagera Suger wataikaribisha Azam Fc kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

No comments:
Post a Comment