BUKOBA SPORTS

Monday, September 3, 2012

MCHEZAJI SWEDEN AANGUKA NA KUFA UWANJANI.

Victor Brannstrom.
MCHEZAJI mmoja wa soka nchini Sweden ameanguka na kufariki kwa kile kinachodaiwa moyo wake kusimama kufanya kazi ikiwa ni dakika moja baada ya kuifungia timu yake bao la ushindi katika mchezo wa ligi uliochezwa Jumapili. Mchezaji huyo anayeitwa Victor Brannstrom mwenye umri wa miaka 29, 
aliifungia bao timu yake ya Pitea ambayo ilikuwa ikicheza na Umedalen dakika nne baada ya mchezo kuanza jana wakati alipokaa chini ghafla na kuanza kugalagala kwa mujibu ya walioshuhudia tukio hilo. Watu wa huduma ya kwanza waliingia uwanjani kujaribu kumsadia mchezaji huyo kwa kumpa huduma ya kwanza kabla ya magari matatu ya wagonjwa kuwasili na kumbeba kumuwahisha Brannstron hospitali ambapo alitangazwa kufariki muda mfupi baadae. Mchezaji huyo ambaye alikuwa akicheza katika klabu ya Helsingborg ambayo inashiriki Ligi Kuu nchini humo, alistaafu soka Januari mwaka huu kufuatia tatizo hilohilo la kuanguka lakini alirejea tena dimbani baada ya vipimo kuonyesha kuwa hakuwa na tatizo kubwa la moyo.Taarifa za awali kutoka hospitali ya Pitea ambako alipelekwa mchezaji huyo zinasema kuwa moyo wake ulisimama kufanya kazi lakini watatoa taarifa zaidi pindi mwili wake utakapofanyiwa uchunguzi wa kitu kilichopelekea kifo chake.

No comments:

Post a Comment