BUKOBA SPORTS

Saturday, September 8, 2012

MOLDOVA 0 ENGLAND 5 VIJANA WA ROY HODGSON WAFANYA KWELI!

England Magoli yote 5 katika picha angalia ilivyokuwa ... chini ni picha ikionesha mtanange ukiendelea jana usiku

Meneja wa Timu ya Taifa ya England, Roy Hodgson, pamoja na Mkongwe wa Timu hiyo, Frank Lampard, wamemmwagia sifa Kiungo Tom Cleverley kwa umiliki wake wa nafasi hiyo kwenye Mechi na Moldova iliyochezwa huko Chisinau hapo jana na England kushinda bao 5-0 katika Mechi yake ya kwanza ya Kundi Hkuwania kwenda Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil.

Akiichezea England Mechi yake ya pili tu, Cleverley, Miaka 23, Kiungo huyo wa Manchester United alianzishwa badala ya mwenzake wa Klabu moja Michael Carrick na kuwa pamoja kwenye nafasi hiyo na Frank Lampard na Steve Gerrard ambe alitolewa baada ya Dakika 45 na kuingizwa Carrick.

Hodgson alisema: “Alicheza vizuri sana Dakika zote 90 na ukitazama utajua kwa nini Sir Alex Ferguson anafurahishwa na Mchezaji huyu!”

Nae Mkongwe Lampard, ambae jana alifunga Bao mbili, amesema: “Ni furaha kucheza na Tom na bado yu Kijana hivi atakuwemo kwenye Timu hii kwa Miaka mingi tu.”

Mbali ya kufurahishwa na Cleverley, pia Hodgson alifurahishwa na Winga wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain ambae alicheza kwa Dakika 60 na kutolewa na nafasi yake kushikwa na mwenzake wa Arsenal Theo Walcott.
Jumanne ijayo England itakuwepo Uwanja wa Wembley Jijini London kucheza na Ukraine katika Mechi yake ya pili ya Kundi H kuwania kwenda Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil.

 Lampard na Steven Gerrard wakipongezana jana usiku baada ya kufanya kazi

 Roy Hodgson (kulia) na Gary Neville (wa tatu kutoka kushoto) kwenye benchi la ufundi la England

Frank Lampard (kushoto) akifurahia ushindi na Tom Cleverley kwenye mtanange wao wa jana usiku wa kufuzu kucheza Katika Mechi za kuwania kwenda Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazi.
MABAO:

-Frank Lampard alifunga dk Penati Dakika ya 3, 29

-Jermaine Defoe alifunga dk 32

-James Milner alifunga dk 74

-Leighton Baines alifunga dk 84

Hapo hapo vigogo hao wa england kushinda pia kulikuwa na mitanange mingi sana ya ulaya, England, Germany, France, jana walishinda Mechi zao za kwanza za Makundi yao lakini Italy walitoka sare na huko Marekani ya Kuisini, Argentina waliichapa Paraguay Bao 3-1 na kuongoza Kundi la Nchi za Marekani ya Kusini.

Messi akusita aliwashukuru mashabiki wake wa Argentina
NAHODHA wa kikosi cha timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi ameonyesha kufurahishwa kwake na ushindi waliopata katika mchezo wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Paraguay na kuwashukuru mashabiki kwa kushangilia katika mchezo huo. Nyota huyo anayecheza katika klabu ya Barcelona mashuti yake yaligonga mwamba mara mbili wakati timu yake ilipoibuka na ushindi wa mabao 3-1 katika Uwanja wa Mario Kempes uliopo jijini Cordoba lakini alifanikiwa kuzifumania nyavu katika kipindi cha pili kwa mpira mzuri wa adhabu aliopiga. Mabao mengine ya timu hiyo yalifungwa na Angel Di Maria na Gonzalo Higuain na kuipaisha Argentina mpaka kileleni mwa msimamo wa timu zitakazofuzu michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2014. Akihojiwa Messi amesema kuwa anajisikia furaha pindi anapoona mashabiki wanawashangilia kwani kunawaongeza nguvu ya kufanya vizuri zaidi. Mshambuliaji huyo mpaka sasa ameshafunga mabao tisa katika mechi tano alizoichezea timu hiyo kwa mwaka huu ambapo katika michezo yote aliyofunga timu yake iliibuka na ushindi. 

No comments:

Post a Comment