BUKOBA SPORTS

Wednesday, September 5, 2012

OWEN AJIUNGA NA KLABU YA STOKE CITY AKIWA AMECHELEWA!

Michael Owen
Mchezaji Michael Owen ambaye ameachiwa huru na klabu ya Man United hatimaye ameweza pata klabu ya kumsajili ambayo ni Stoke City.
Lakini utata unakuja hapa,Stoke walishapeleka majina 25 ya wachezaji ambao watashiriki katika kuichezea klabu hiyo katika msimu huu wa ligi ya Uingereza na hivyo kulazimika kuiomba Premier League ikubali kufutwa kwa mchezaji mmoja ili nafasi yake aichukue Owen.

Sheria ambazo zinaiongoza Ligi hiyo ya Uingereza haina sheria kama hiyo ya kutoa ruhusa ya mtu afutwe ili awekwe mwingine. Kwa hiyo majadiliano ndiyo yanafanyika ya aidha akubaliwe au akataliwe.
Mchezaji ambaye anatakakufutwa ni kiungo Tonge mwenye umri wa miaka 29.
Owen mwenyewe kupitia mtandao wa twitter alisema,
“Nina furaha kujiunga na Stoke, kilichobakia ni kwa Premier League wanipe ruhusa ili niweze cheza. Ninashauku ya kufanya kazi chini ya kocha Tony Pulis. Ameandaa kikosi kizuri na ninashauku wa kuanza cheza.”

No comments:

Post a Comment