BUKOBA SPORTS

Tuesday, September 4, 2012

REAL MADRID YAMCHEFUA CRISTIANO RONALDO, ATOA MWANYA KWA MAN UNITED, CITY NA PSG!

KLABU ya Real Madrid ya Hispania imeanza kumchefua mshambuliaji wake Cristiano Ronaldo, Jambo ambalo limemfanya jumapili iliyopita kufunga bao lake la 150 akiwa Real Madrid, lakini aligoma kushangilia.
Ronaldo amekuwa mchezaji wa tisa kwa kufunga mabao mengi katika historia ya Real Madrid. Ronaldo alielezea kuwepo na mpasuko kati yake na wachezaji wenzake katika klabu hiyo.
Mshambuliaji huyo nyota wa kimataifa wa Ureno na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameziweka klabu za Manchester United na City kujiweka tayari kumsajili baada ya kukiri kuwa anataka kuondoka Madrid. Chanzo kimoja cha habari nchini Hispania kilihabarisha kuwa nyota huyo alimwambia rais wa Madrid kuwa anataka kuondoka kwa kile kilichodaiwa kushindwa kuelewana na baadhi ya wachezaji wenzake. Hali hiyo ya kutokuwa na furaha kwa Ronaldo mwenye umri wa miaka 27 ilionekana wazi wakati wa mchezo wa Jumapili baina ya Madrid na Granada ambapo alishinda mabao mawili lakini hakushangilia.
Akihojiwa kuhusiana na tukio hilo nyota huyo amesema kuwa alikuwa katika majonzi na viongozi wa klabu hiyo wanajua sababu hivyo hawezi kusema zaidi kuhusiana na hilo.Kauli hiyo inazitamanisha klabu za United, City pamoja na Chlesea kumsajili mchezaji huyo ambapo hivi sasa watakuwa wakifuatilia mstakabali wa mchezaji huyo katika klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment