BUKOBA SPORTS

Tuesday, September 4, 2012

ROBIN VAN PERSIE AWAOMBA RADHI MASHABIKI WA MAN UNITED BAADA YA KUKOSA PENATI

ROBIN van Persie alipiga hat-trick kuisaidia Manchester united kutoka nyuma na kupata ushindi wake muhimu kabisa katika mechi ya Ligi kuu England juzi, lakini baadaye aliwaomba radhi mashabiki wa Man united kutokana na kukosa kwake penati katika mchezo huo.Hadi sasa Rvp ana jumla ya magoli manne(4) aliyofunga kwenye mechi mbili alizocheza tangu ligi kuu England ianze. alibainisha kusikitishwa na kitendo cha kukosa penati wakati timu yake ilikuwa nyuma ya goli 2-1 dhidi ya timu ya Southampton.
RVP alisema.. "Magoli matatu niliyofunga yana maana ya pointi tatu, lakini bado nahisi kuchaganyikiwa kidogo. sijuhi ni kitu gani nilikuwa nafikiria wakati napiga ile penati."

No comments:

Post a Comment