Wakipongezana

Neymar (kushoto) akichuana na mchezaji wa Japan leo.
POZNAN, Poland
Brazil walitawala mechi nzima waliyocheza ugenini kuanzia saa 9:10 alasiri leo na kushinda 4-0 katika mechi yao ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Japan mjini Poznan, Poland leo Jumanne.
Paulinho alifunga goli la utangulizi katika dakika ya 12 kutokana na shuti kali alilopiga kutoka umbali wa yadi 20, kabla Neymar hajaongeza la pili kwa njia ya penati katika dakika ya 29.
Katika kipindi cha pili, Brazil waliongeza mashambulizi na straika wa Santos, Neymar akafanya ubao wa magoli usomeke 3-0, kabla Kaka aliyeonyesha kiwango cha juu hajafunga bao la nne kuelekea mwisho wa mechi hiyo.
Kaka alianza tena kikosini katika kikosi kilichoonekana kuwa ni kile kile cha kocha Mano Menezes, ambaye alibadili mchezaji mmoja tu kutoka katika timu iliyoanza dhidi ya Iraq na kushinda 6-0, akianza Leandro Castan badala ya majeruhi Marcelo.
No comments:
Post a Comment