BUKOBA SPORTS

Tuesday, October 16, 2012

FIFA KUIKAGUA RECIFE TENA.

TIMU ya ukaguzi kutoka Shirikisho la Soka Duniani-FIFA leo inatarajiwa kutembelea mji wa Recife kabla ya kuamua kuujumuisha mji uliopo Kaskazini-Mashariki mwa Brazil katika michuano ya Kombe la Shirikisho mwakani. Hatua hiyo imekuja ikiwa ni mwezi mmoja kabla ya FIFA kutangaza viwanja vitakavyotumika kwa ajili ya michuano hiyo ambayo hutangulia kabla ya Kombe la Dunia. Recife ni mojawapo ya miji sita iliyoteuliwa kuwa wenyeji wa michuano hiyo lakini itathibisha ushiriki wake kama wataonyesha kiwango kizuri cha maandalizi ingawa kamati ya maandalizi ya mji huo ilitamba kuwa wakaguzi hao watafurahia watakachokiona katika ziara hiyo.Mbali na kutembelea mji huo, pia Katibu Mkuu wa FIFA Jerome Valcke ataanza ziara yake ya kutembelea miji ya Belo Horizonte na Porto Alerge kabla ya kuhudhuria kikao cha bodi ya kamati ya maandalizi kitakachofanyika jijini Rio de Janeiro. 


VIWANJA HUKO BRAZIL VITAKAVYOTUMIKA 2014 KOMBE LA DUNIA.

São Paulo Arena, São Paulo, Brazil


Arena Pantanal, Cuiabá, Brazil

Arena Pernambuco, Recife, Brazil

Estádio Nacional de Brasília, Brasília, Brazil

Castelão, Fortaleza, Brazil

Estádio das Dunas, Natal, Brazil

Arena da Amazônia, Manaus, Brazil

In the Arena Fonte Nova, Salvador, Brazil
Arena Fonte Mineirão, Belo Horizonte, Brazil

Mineirão, Belo Horizonte, Brazil






No comments:

Post a Comment