Refa
wa Spain Mateu Lahoz amefungiwa baada ya kubainika kuwa alifanya makosa
kwenye Mechi ambayo Barcelona iliifunga Sevilla Dakika za mwisho Bao
3-2 kwenye Mechi ya La Liga.
Chama cha Soka cha Spain, RFEF,
kimemuadhibu Refa huyo kwa kumtoa nje kwa Kadi Nyekundi Mchezaji wa
Sevilla Gary Medel baada ya kuvaana na Cesc Fabregas na pia kumtoa nje
Kocha wa Sevilla Michel.
Pia Refa huyo amehukumiwa kwa kutokuona
mpira ulioshikwa kwa mkono na Thiago wakati Barcelona wanaenda kufunga
bao lao la ushindi kupitia David Villa.
RFEF imeamua kuwa makosa hayo hasa lile la kutolewa Gary Medel halikustahili na hivyo kumwadhibu Refa huyo.
Taarifa ya RFEF imesema: “Kulikuwa na
kuvutana kwa Wachezaji wawili na wakagusana Vichwa bila kupigana kwa
nguvu lakini Mchezaji mmoja akahadaa kapigwa. Gary Medel akatolewa na
hilo ni kosa la kiufundi na halikustahili.”
Refa Mateu Lahoz sasa atatumikia Kifungo
cha Mechi moja na ataikosa Mechi aliyopangiya ya Real Madrid v Celta
Vigo hapo Oktoba 20.
Hadi sasa Barcelona ndio wanaongoza La
Liga kwa kushinda Mechi 6 na sare moja waliyotoka na Mahasimu wao Real
Madrid bao 2-2 Jumapili iliyopita.
Ligi hiyo kwa sasa ipo kando kupisha
Mechi za Kimataifa zilizopo kwenye Kalenda ya FIFA na iatarudi tena
kuanzia Wikiendi ya Oktoba 20.
No comments:
Post a Comment