>>BADO MSHIKA REKODI MAGOLI: Man United 249, England 49!!
Nguli
Sir Bobby Charlton leo anasherehekea Siku yake ya kuzaliwa kwa kutimiza
Miaka 75 huku akiwa bado anashikilia Rekodi ya kuwa Mfungaji Bora wa
Manchester United, Mabao 249, na Timu ya Taifa ya England, Mabao 49,
huku pia akiwa ni mmoja wa Waingereza wawili tu, mwingine ni Nobby
Stiles ambae pia alichezea Man United, kushinda kwa pamoja Kombe la
Dunia [Na England 1966] na Kombe la Klabu Bingwa Ulaya [Na Man United
1968].
Sir Bobby Charlton ambae alikuwa ni
Kiungo, pamoja na Kaka yake Jackie Charlton aliekuwa Mchezaji wa Leeds
United, walikuwemo kwenye Timu ya England iliyoshinda Ubingwa wa Dunia
walipotwaa Kombe la Dunia Mwaka 1966 Uwanjani Wembley, London.
Alianza kuichezea Manchester United
Mwaka 1956 na Mwaka 1958 alinusurika kwenye ajali ya Ndege iliyowabeba
Timu ya Man United huko Munich, Germany na kuwaua Wachezaji kadhaa wa
Timu hiyo.
MENEJA NGULI wa Man United, Sir Matt Busby alitamka:
“Kitu kikubwa kwa Meneja ni
kuamini vipaji alivyonavyo. Bobby Charlton hakusaliti imani hiyo.
Ilikuwa ni tunu kuwa nae kuichezea Timu yako!”
Sir Bobby Charlton ameichezea Man United
Mechi 606 kati ya Mwaka 1956 na 1973 na ndie aliekuwa akishikilia
rekodi ya kuichezea Mechi nyingi Klabu hiyo hadi ilipovunjwa na Ryan
Giggs Tarehe 6 Machi 2011.
Mwaka 1994 alitunukiwa Cheo cha Sir na MalkIa Elizabeth wa Uingereza.
No comments:
Post a Comment