kwakuwa nahodha mkuu Steven Gerrad ambayeamesimamishw kwa michezo kazaa na nahodha msaidizi Frank Lampad hawata wai mechi iyo kutokana na majera ya goti waliyo yapata,Rooney apo awali alishawahi kuingoza timu iyo kwa kipindi kifupi ambacho England ilicheza na Brazil walipofungwa akiwakama nahodha pia ikumbukwe kuwa Rooney toka apewe unahodha Engand haijawi kushinda mechi hata moja na kama watashinda basi itakuwa ni mara ya kwanza kwa Rooney na nahodha Steven Gerrad anatarajiwa kurudi katika game yao na Poland.
______________________________________
JOAN MINJA APINGWA NA WADAU SITA KUGOMBEA UONGOZI CHA CHA MPIRA WANAWAKE TANZANIA 'TAWFA'
Wagombea
sita wa nafasi mbalimbali za uongozi katika Chama cha Mpira wa Miguu wa
Wanawake Tanzania (TWFA) wamewekewa pingamizi na wadau wa mchezo huo.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TWFA, Ombeni Zavala,
wagombea hao ni Joan Minja anayewania nafasi ya Mwenyekiti ambaye
amewekwa pingamizi na wadau sita. Pia Isabellah Kapera ambaye anagombea
uenyekiti amewekewa pingamizi moja.
Wagombea
watatu wa nafasi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) nao wamewekewa pingamizi. Wagombea hao ni Julliet
Mndeme (pingamizi sita), Zena Chande (pingamizi nne) na Jasmin Soud
mwenye pingamizi tatu.
Naye Rahim Maguza anayewania ujumbe wa Kamati ya Utendaji amewekewa pingamizi moja.
Licha
ya pingamizi hizo, wagombea wote wanatakiwa kuhudhuria usaili wakiwa na
vyeti vyao halisi vya kitaaluma utakaofanyika Oktoba 12, 13 na 14 mwaka
huu kwenye ofisi za TFF zilizopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es
Salaam kuanzia saa 3 asubuhi.
________________________________
SIMBA YAELEKEA TANGA BILA YA NGASA, OKWI NA REDONDO.
Mabingwa
watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara Simba ya jijini Dar es Salaam
imeondoka jijini hii leo na kuelekea jijini Tanga kwa ajili ya mchezo
wao wa raundi ya saba dhidi ya Coast Union ya huko mchezo ambao
unatarajiwa kuchezwa katika uwanja wa Mkwakwani Oktoba 13.
Simba
wameelekea Tanga wakiwa ndio vinara wa ligi hiyo ya Tanzania Bara
inayoshirikisha jumla ya timu 14 huku Simba wakiongoza baada ya
kujikusanyia jumla ya alama 16 wakifuatiwa na Azam fc yenye alama 14.
Simba
imeondoka bila ya wachezaji wake kadhaa muhimu akiwepo Mrisho Ngasa
anayesumbuliwa na malaria kama ilivyo kwa Ramadhani Chombo Redondo
ambaye naye anasumbuliwa na malaria.
Wengine walioachwa ni Haruna
Shamte ambaye anasumbuliwa na enka, Kiggi
Makassi mwenye matatizo ya goti pamoja na Abdalah Seseme na Waziri Hamadi.
Kwa upande wa mganda Emmanuel Okwi yeye anaelekea kwao Uganda kwa ajili ya majukumu ya kimataifa.
MAKIPA:Juma Kaseja na Wilbert Mweta.
Walinzi: Chollo, Maftah, Nyoso, Paschal Ochieng, Kapombe, Hassan Khatib, Paulo Ngalema, Koman Keita.
Viungo: Kazimoto, Jonas Mkude, Kiemba, Salim Kinje, Ramadhani Singano, Uhuru Selemani, Boban.
Washambuliaji:Sunzu, Edward Christopher, Haroun Chanongo, Daniel Akuffo na Abdallah Juma.
RATIBA RAUNDI YA 7
10.10.2012. | 43 | KAGERA SUGAR | JKT RUVU | KAITABA | KAGERA | |
11.10.2012. | 44 | TOTO AFRICANS | YOUNG AFRICANS | CCM KIRUMBA | MWANZA | |
13.10.2012. | 45 | POLISI MOROGORO | AZAM | JAMUHURI | MOROGORO | |
13.10.2012. | 46 | TANZANIA PRISONS | JKT OLJORO | SOKOINE | MBEYA | |
13.10.2012. | 47 | COASTAL UNION | SIMBA | MKWAKWANI | TANGA | |
13.10.2012. | 48 | RUVU SHOOTINGS | AFRICAN LYON | MABATINI | PWANI | |
13.10.2012. | 49 | MTIBWA SUGAR | MGAMBO JKT | MANUNGU | MOROGORO |
___________________________________________
VERMAELEN ANA AMINI WILSHERE NI MIONGONI MWA VIUNGO BORA DUNIANI.
Thomas
Vermaelen anaamini kuwa Jack Wilshere ana uwezo wa kuwa mmoja kati ya viungo
hodari dunaini.
Kiungo huyo
alikuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi 14 akisumbuliwa na maumivu ya enka na
mguu lakini amerejea akiwa vizuri katika kikosi cha timu ya taifa ya wachezaji
wenye umri chini ya miaka 21.
Amenukuliwa na
mtandao wa klabu hiyo akisema Vermaelen akisema,
"unajua
alichokifanya katika msimu wake mzima wa kwanza akiwa na Arsenal, alifanya vitu
vikubwa sana”.
"kwa
upande wangu anaweza kuwa mmoja kati ya viungo bora kabisa duniani. Ana uwezo
mkubwa wa kufikia hapo.
"ninafuraha
sana amerejea sasa. Anafanya kazi ya kurejesha uwezo wake kama zamani na hilo
ni jambo muhimu. Nadhani baadaye ataibeba timu hii."
________________________________
VILLA SQUAD YAJIANDAA NA LIGI DARAJA LA KWANZA
Kikosi cha timu ya Villa squad
Fc wakijifua kwa ajiri ya kujiandaa na ligi ya Taifa daraja la kwanza,
inayotarajia kuanza Octoba 20.
kikosi hicho kinajiandaa vizuri mazoezi yake kwenye uwanja wa barafu magomeni.
Akizungumza na Rockersports, ofisa habari wa villa, Andrew Chale, amesema wachezaji wake wako katika morali
ya hali ya juu kuakikisha wanarudi ligi kuu, ili kuendeleza ushindani.
"tumedhamiria
na tunaweza, villa tupo fiti licha ya changamoto tulizo nazo ila
tutapambana mpaka hatua ya mwisho na kurudi ligi kuu msimu ujao".
Chale
ameomba mashabiki na wadau wa Villa kujitokeza kwa wingi kwenye mazoezi
ya timu hiyo kwenye shule ya Lions Magomeni na kuipa sapoti na kutoa
morali zaidi kwa vijana pamoja na kuchaingia timu hiyo.
Aidha,
Chale amesema kuwa, Ijumaa hii kutakuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya
timu ya COSMOS POLITAN FC ya Kariakoo, mchezo wa kujipima nguvu
utakaochezwa uwanja wa makulumla maarufu kama kines
___________________________________NGASSA, RIDONDO KUIKOSA COASTAL KUTOKANA NA MAJERUHI.
KLABU ya soka ya Simba inatarajia kuwakosa wachezaji wake nyota katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya Coastal Union ya Tanga Jumamosi.
Wachezaji watakaokosa mchezo huo utakaopigwa katika Uwanja wa Mkwakwani ni pamoja na Mrisho Ngassa na Ramadhani Chombo “Ridondo” ambao wanasumbuliwa na malaria, Haruna Shamte anayesumbuliwa na enka pamoja na Kiggi Makassi anayesumbuliwa na goti. Wengine ni Emmanuel Okwi aliyeitwa katika timu yake ya taifa ya Uganda, Abdallah Seseme na Wazir Hamad. Wachezaji ambao watasafiri na timu hiyo ni pamoja na makipa Juma Kaseja, Wilbert Mweta mabeki ni Chollo, Maftah, Nyoso, Paschal Ochieng, Kapombe, Hassan Khatib, Paulo Ngalema, Koman Keita. Viungo ni Kazimoto, Jonas Mkude, Kiemba, Salim Kinje, Ramadhani Singano, Uhuru Selemani, Boban akati washambuliaji watakuwa Sunzu, Edward Christopher, Haroun Chanongo, Daniel Akuffo na Abdallah Juma.
No comments:
Post a Comment