IFUATAYO NI TAARIFA KAMILI:
Release No. 168
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Oktoba 15, 2012
13 WAPITISHWA KUGOMBEA UONGOZI TWFA
Wagombea 13 kati ya 15 waliojitokeza
kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye Chama cha Mpira wa Miguu wa
Wanawake Tanzania (TWFA) wamepitishwa baada ya usaili uliofanyika juzi.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya
Uchaguzi ya TWFA, Ombeni Zavala, waliopitishwa kwenye nafasi ya
uenyekiti ni Isabellah Huseein Kapera, Joan Ndaambuyo Minja na Lina Paul
Kessy.
Makamu Mwenyekiti ni Rose Kisiwa wakati
wanaowania nafasi ya Katibu Mkuu ni Amina Ali Karuma na Cecilia Oreste
Makafu. Mgombea pekee wa nafasi ya Katibu Msaidizi, Macky Righton Mhango
naye amepita kwenye usaili huo. Aliyepitishwa kwenye nafasi ya Mhazini
ni Rose Stewart Msamila.
Furaha Francis na Zena Chande
wamepitishwa kuwania nafasi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakati waliopita kuwania ujumbe wa Kamati
ya Utendaji ya TWFA ni Triphonia Ludovick Temba, Rahim Salum Maguza na
Sophia James Charles.
Hivi mchakato wa uchaguzi wa TWFA uko
katika kipindi cha kukata rufani ambapo ni kuanzia Oktoba 15-17 mwaka
huu. Rufani zinatakiwa zifike kwa Katibu Mkuu wa TFF kabla ya saa 10
kamili jioni ya Oktoba 17 mwaka huu.
Wagombea wawili ambao hawakupitishwa kwa ajili ya uchaguzi huo
unaotarajiwa kufanyika Novemba 4 mwaka
huu ni Julliet Mndeme na Jasmin Soud walioomba ujumbe wa Mkutano Mkuu wa
TFF. Wagombea hao ambao pia walikuwa wamewekewa pingamizi hawakufika
kwenye usaili.
PONGEZI KWA UONGOZI MPYA ARFA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa
wa Pwani (COREFA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika jana (Oktoba
14 mwaka huu).
Ushindi waliopata viongozi
waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi wajumbe wa Mkutano
Mkuu wa COREFA walivyo na imani kubwa kwao katika kusimamia mchezo huo
mkoani Pwani.
TFF inaahidi kuendeleza ushirikiano wake
kwa Kamati ya Utendaji ya COREFA chini ya uenyekiti wa Hassan Othman
Hassan ambaye amechaguliwa tena kuongoza chama hicho.
Uongozi huo mpya una changamoto nyingi,
kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha shughuli za mpira wa miguu mkoani
Pwani kwa kuzingatia katiba ya COREFA pamoja na vyombo vya mpira wa
miguu vilivyo juu yake.
Pia tunatoa pongezi kwa Kamati ya
Uchaguzi ya COREFA na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi
huo unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF.
Viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi
huo ni Hassan Othman Hassan (Mwenyekiti), Riziki Majala (Katibu),
Geofrey Irick Nyange (Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF), Juma Haruna Kisoma
(Mwakilishi wa Klabu TFF) na Abubakar Allawi (Mhazini).
Waliochaguliwa kuwa Wajumbe wa Kamati ya
Utendaji katika uchaguzi huo uliofanyika kisiwani Mafia ni Musa Bakari
Athumani, Godfrey Magnus Haule na Gwamaka Oden Mlagila. Mwakilishi wa
Wanawake ni Florence Ambonisye.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment