BUKOBA SPORTS

Monday, October 15, 2012

WORLD CUP 2014 BRAZIL QUALIFIERS: SPAIN V FRANCE

>>Iniesta ndani kwa Spain!!
>>FRANCE yapagawishwa kufungwa na Japan!!
KESHO Jumanne, Mjini Madrid, Mabingwa wa Dunia na Ulaya, Spain, wanaikaribisha France kwenye Mechi ya Kundi I la Kanda ya Ulaya kusaka nafasi kucheza Kombe la Dunia Mwaka 2014 na kitu pekee kinachomuumiza kichwa Kocha wa Spain, Vicente Del Bosque, ni nani ampange wakati France wao wameweweseka baada ya kuchapwa bao 1-0 na Japan kwenye Mechi ya Kirafiki hivi juzi.
Juzi, wakicheza Stade de France Mjini Paris, France walifungwa bao 1-0 na Japan katika Mechi ya Kirafiki, kwa bao lililofungwa mwishoni na hicho ni kichapo cha kwa kwanza kwa Kocha Didier Deschamps tangu aitwae Timu kutoka kwa Laurent Blanc mara baada ya kutolewa kwenye Robo Fainali ya EURO 2012 walipochapwa na Spain.
France watakwenda huko Madrid bila ya Viungo wa Wakabaji, Abou Diaby na Rio Mavuba, ambao wameumia lakini pia kitu kinachowapa fadhaa ni kuendelea kwa ukame wa magoli kwa Straika wao Karim Benzema ambae amefunga bao 15 tu katika Mechi 53 alizochezea Spain.
Kwa Spain, hali ni murua hasa baada ya kushinda ugenini katika Mechi yao ya pili ya Kundi I walipoitandika Belarus bao 4-0 na kutwaa uongozi wa Kundi hilo kwa tofauti ya magoli mbele ya France.

MSIMAMO
KUNDI I
1 Spain Mechi 2 Pointi 6 [Tofauti ya Magoli 5]
2 France Mechi 2 Pointi 6 [Tofauti ya Magoli 5]
3 Georgia Mechi 3 Pointi 4
4 Finland Mechi 2 Pointi 1
Belarus Mechi 3 Pointi 0
 
Kocha wa Spain, Vicente Del Bosque, ambae alimchezesha Kiungo Sergio Busquets kama Sentahafu na kumpa namba Kiungo wa Arsenal, Santi Cazorla, kwenye Mechi na Belarus, anatarajiwa kufanya mabadiliko kwa ajili ya Mechi na France na kumweka Raul Albiol kama Sentahafu na pia kumchezesha Kiungo Andres Iniesta ambae hakucheza na Belarus.
Mechi hii ya Jumanne kati ya Spain na France inazikutanisha Timu zote zenye Pointi 6 kila mmoja na kila Timu inataka ushindi ili kupita moja kwa moja kwenda Fainali za Kombe la Dunia kama Mshindi wa Kundi.

VIKOSI VINATARAJIWA:
Spain: Iker Casillas; Alvaro Arbeloa, Sergio Ramos, Raul Albiol, Jordi Alba; Sergio Busquets, Xabi Alonso, Pedro, Xavi, Andres Iniesta, Cesc Fabregas
France: Hugo Lloris; Mathieu Debuchy, Laurent Koscielny, Mamadou Sakho, Patrice Evra; Moussa Sissoko, Yohan Cabaye, Blaise Matuidi; Franck Ribery, Karim Benzema, Jeremy Menez

RATIBA MECHI ZIJAZO
Jumanne Oktoba 16
[SAA za BONGO]
Albania v Slovenia
Andorra v Estonia
Belarus v Georgia
Belgium v Scotland
Bosnia-Hercegovina v Lithuania
Czech Republic v Bulgaria
Hungary v Turkey
Iceland v Switzerland
Israel v Luxembourg
Latvia v Liechtenstein
Macedonia v Serbia
Portugal v Northern Ireland
Romania v Netherlands
Russia v Azerbaijan
San Marino v Moldova
Slovakia v Greece
Spain v France
Ukraine v Montenegro
2000 Cyprus v Norway
2100 Faroe Islands v Rep of Ireland
2130 Austria v Kazakhstan
2130 Croatia v Wales
2145 Germany v Sweden
2145 Italy v Denmark
2200 Poland v England

FAHAMU:
-ULAYA yapo Makundi 9
-Washindi 9 wa kila Kundi wataingia Fainali moja kwa moja na Washindi wa Pili 8 bora wenye rekodi nzuri dhidi ya Timu zilizomaliza nafasi za Kwanza, Tatu, Nne na Tano kwenye Kundi lao watapelekwa kwenye Droo kupanga Mechi 4 za Mchujo, zitakazochezwa nyumbani na ugenini, ili kupata Timu nne zitakazoingia Fainali.

No comments:

Post a Comment