BUKOBA SPORTS

Sunday, October 14, 2012

MAGDALENA ROY ANYAKUA TAJI LA TOP MODEL REDD'S MISS TANZANIA


MREMBO wa Ilala, Magdalena Roy, usiku wa kuamkia leo amefanikiwa kunyakua taji la mrembo wa pili kuingia hatua ya nusu fainali ya Redd's Miss Tanzania 2012 baada ya kuwashinda warembo wengine 29 na kutwaa taji la Top Model. Magdalena aliibuka mshindi katika shindano dogo la Redd's Miss Tanzania lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika Hoteli ya Kimataifa ya Naura Springs jijini Arusha. Kwa matokeo hayo Top Model, Magadalena Roy anaungana na Miss Photogenic, Lucy Stephano katika nusu fainali hiyo na kukaa tayari kusubiri warembo wengine 13 watakaoungana katika Nusu fainali hizo.Hongera sana Roy!!
Mrembo kutoka Mara EUGENE FABIAN na yeye amefanikiwa kunyakuwa Taji la Ubalozi wa Hotel ya Naura Spring ya jijini Arusha. Awali taji hili lilikuwa likishikiliwa na Neema Joel.
           "HONGERA SANA EUGENE FABIAN!!
    WWW.BUKOBASPORTS.COM INAKUPA PONGEZI KWA HATUA HIYO.

No comments:

Post a Comment