Hapo hakuna Udini, Ukabila, Urafiki wala Ushikina; kutoka kushoto ni
Marehemu Habib Halala, Mzee Paul Soizgwa, JK Nyerere, Brig. Hashim
Mbita, Mzee Mkapa, siku kumi kabla ya JK kustaafu uraisi 1985.
Leo ni kumbukumbu ya Baba waTaifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Waziri Mkuu na Rais wa kwanza wa Tanzania (13 Aprili 1922 – 14 Oktoba1999)
Hayati Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julias Kambarage Nyerere
Afikisha Miaka 13 Tangu Kifo Chake
JULIAS Kambarage Nyerere alizaliwa mwaka 1922
(katika kijiji cha Butiama, wilaya ya Musoma, Mkoa wa Mara, Tanzania
(wakati ule: Tanganyika). Alikuwa mojawapo kati watoto 26 wa Nyerere
Burito, chifu wa kabila la Wazanaki. Alipokuwa mtoto Nyerere alichunga
mifugo ya babake; katika umri wa miaka 12 aliingia shule akitembea
kilomita 30 hadi Musoma. Baada ya kumaliza shule ya msingi aliendelea
kusoma shule ya wamisionari Wakatoliki huko Tabora. Katika umri wa miaka
20 alibatizwa akawa mkristo Mkatoliki hadi mwisho wa maisha yake.
Aliporejea Tanganyika kutoka masomoni, Nyerere alifundisha Historia,
Kingereza na Kiswahili katika shule ya St. Francis iliyo karibu na Dar
es Salaam. Mwaka 1953 alichaguliwa kuwa raisi wa chama cha Tanganyika
African Association (TAA), chama ambacho alikisaidia kukijenga alipokuwa
mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Makerere. Mwaka 1954 alikibadilisha
chama cha TAA kwenda katika chama cha Tanganyika African National Union
(TANU) ambacho kilikuwa cha kisiasa zaidi kuliko TAA. Ndani ya mwaka
mmoja chama cha TANU kilikuwa tayari chama cha siasa kinachoongoza
Tanganyika.
Uwezo wake wa kimaongezi na kuunganisha watu ulimwezesha kufanikisha
Tanganyika kupata uhuru bila umwagaji wa damu. Ushirikiano mzuri
aliouonyesha aliyekuwa gavana wa wakati huo bwana Richard Turnbull
ulisaidia pia kuharakisha upatikanaji wa uhuru. Nyerere aliingia katika
bunge la kikoloni mwaka 1958 na kuchaguliwa kuwa waziri mkuu mwaka 1960.
Februari 05, 1977 aliongoza chama cha TANU katika tendo la kuungana
na chama tawala cha Zanzibar ASP na kuanzisha chama kipya cha CCM (Chama
cha Mapinduzi) akiwa mwenyekiti wake. Nyerere aliendelea kuongoza Taifa
hadi 1985 alipomwachia nafasi raisi wa pili Ali Hassan Mwinyi.
Aliendelea kuongoza Chama cha CCM hadi 1990 na kuwa na athari kubwa
katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake.
Serikali ilipotangaza rasmi kwamba Nyerere hatunaye tena, uchungu na simanzi uliikumba nchi nzima na dunia kwa ujumla hususani kwa wale waliokuwa wanamjua Nyerere na kujua alichokuwa akikisimamia na alichokiamini. Bara la Afrika likawa limempoteza kipenzi chake, mtoto wa Afrika ambaye thamani ya mchango wake katika ukombozi wa bara la Afrika haina kipimo. Mpaka anafariki dunia alikuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha amani barani Afrika.Mfano mzuri ni mgogoro wa Burundi aliokuwa akijaribu kuusuluhisha. Mwenyewe aliwahi kutamka kwamba yeye ni mwafrika kwanza na kisha mjamaa.
Lakini je,sote tunafahamu japo kidogo tu historia ya Mwalimu Nyerere? Uwezekano ni kwamba sio wote,hususani vijana wa sasa. Kwa kifupi na kwa msaada wa vyanzo mbalimbali hii hapa historia fupi ya Hayati Baba wa Taifa;
WWW.BUKOBASPORTS.COM TUTAKUKUMBUKA DAIMA!!!
Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere alizaliwa tarehe 13 Aprili mwaka 1922 huko
Butiama mkoani Mara, pembezoni mwa ziwa Victoria,kaskazini mwa Tanzania.
Baba yake alikuwa ni Chifu katika kabila dogo la Wazanaki.Nyerere
alikuwa miongoni wa watoto wanaosemekana kufikia hadi 26. Baba yake,
Mzee Burito Nyerere alikuwa na wake wapatao 22.Alianza shule akiwa na
umri wa miaka 12 (ilimbidi kutembea kwa zaidi ya kilometa 26 hadi Musoma
mjini ili kupata elimu ya msingi). Kipaji cha uelewa shuleni
kilimuwezesha kumaliza kozi ya miaka minne ndani ya miaka mitatu tu.
Baadaye mnamo mwaka 1937,alijiunga na shule ya sekondari ya serikali ya
Tabora kwa masomo ya sekondari. Alibatizwa katika kanisa katoliki akiwa
na umri wa miaka 20.Kipaji chake cha kitaaluma na kiuongozi kilionekana tangu mapema. Kwa msaada wa waliokuwa waalimu wake pale Tabora (ma-father wa kanisa katoliki) baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda kusomea ualimu. Fikra za kimapinduzi na kusaidia waafrika wenzake zilianza kuonekana wazi akiwa Makerere.
Kazi
ya kuviunganisha vikundi mbalimbali vya kisiasa vilivyokuwa vimeanza
kutapakaa nchi nzima haikuwa rahisi. Lakini alifanikiwa kufanya hivyo
mwaka 1954 kwa kuundwa kwa TANU(Tanganyika African National Union) na
yeye kuchaguliwa kukiongoza.
Humo ndimo alimopumzika Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.Tizama na tafakari kwa makini maneno yaliyoandikwa hapo nje.
Aliingia
katika bunge la wakati huo mwaka 1958 kabla hajawa waziri mkuu mwaka
1960. Tarehe 1 May 1961, Tanganyika ilipewa uhuru wa kujitawala na
Nyerere akawa waziri mkuu wa kwanza. Uhuru kamili ulipatikana mwaka
tarehe 9 December 1961. Mwaka mmoja baadaye (1962) Nyerere akawa Raisi
wa kwanza wa Tanganyika ilipokuwa Jamhuri ya Tanganyika.
Mwalimu Nyerere(katikati),mama yake
mzazi(kushoto) na mkewe Maria(kulia).Picha hii ilipigwa Novemba 10,1985
Butiama baada ya Nyerere kustaafu.
Julius
Nyerere alimuoa Maria Gabriel Magige (Mama Maria Nyerere) tarehe 24
Januari 1953 na walijaliwa kupata watoto wanane. Alipostaafu nafasi yake
ya uraisi mwaka 1985 alirudi kijijini Butiama ambako alibakia kuwa
mkulima wa kawaida mpaka kufariki kwake Oktoba 14, 1999. Endelea
kupumzika kwa amani Mwalimu.
Sura ya Nyerere katika noti ya Shs 100 enzi hizo.
R.I.P MWALIMU JULIUS K.NYERERE.
____________________________________________________
NANI ALIKUWEPO KUMKUMBUKA MWALIMU?
JENERALI ULIMWENGU NA KAZI ZA MWALIMU
Jenerali Ulimwengu anapewa nafasi ya kuzungumzia kazi za Mwalimu Nyerere. Anaanza kwa kusema huwezi kuzungumzia kazi za Mwalimu katika muda wa dakika thelathini ambazo waratibu wa kumbukumbu hii wamempatia. Anasema atakachozungumzia yeye ni kama dibaji tu ya kazi za Mwalimu.
Anaanza kwa kusema kuwa ukitaka kuzungumzia kazi za Mwalimu ni lazima kichwani kwako uelewe kuwa Mwalimu alikuwa ni mtu mwenye kupenda kubadilika, anasema hadi Mwalimu anafariki katika umri wake mkubwa aliokuwa nao, akili yake bado iliweza kufikiri kileo. Anatoa mfano kuwa wakati kuna watu wengi ndani ya CCM, ambacho kilikuwa ni chama cha Mwalimu hadi mauti yanamkumba, kilikuwa kikipinga kabisa kabisa ujio wa sera ya vyama vingi, Mwalimu hakuona aibu kusimamia kidete ujio wa mabadiliko yale kwani alikwishaona wimbi la mabadiliko yaliyokuwa yakitokea ulimwenguni. Jenerali anasema kuwa, “Usisahau kuwa Mwalimu alikuwa ni kiongozi wa kwanza kufutilia mbali mfumo wa vyama vingi hapa nyumbani lakini muda wake ulipopita hakuona haya kusema kuwa jitayarisheni kwa mabadiliko.”
PROFESA ISSA SHIVJI ALIVYOMKUMBUKA MWALIMU
Katika kumjadili Mwalimu, Shivji anaanza kwa kusema, “Huu si tu mwaka wa 8 toka Mwalimu kufariki bali pia ni mwaka wa 40 tangu kuzaliwa kwa Azimio la Arusha. Mbona wote tumesahau basi kukumbuka kuuawa pia kwa Azimio? Hata Taasisi ya Mwalimu pia imesahau hilo, ingekumbuka ingetutahadharisha katika kutengezeza kauli mbiu ya kumkumbuka Mwalimu na marehemu mwanae, Azimio la Arusha.”
No comments:
Post a Comment